
Tanzania kupitia mradi wa Digital Inclusion Project unatekelezwa na shirika la Internet Society Tanzania(ISOC-TZ) katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Kilimanjaro imetwaa tuzo baada ya kujenga uwezo mifumo ya majiji janja (Smart Cities) duniani.
Katika tuzo hizo zilizofanyika nchini Dubai, Rais wa Shirika la ISOC-TZ, Nazar Nicholas baada ya kupokea tuzo hiyo alisema huu ni uthibitisho kuwa kuna mambo mazuri yanayofanyika nchini Tanzania chini ya Rais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Alisema sera nzuri zinazotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio zinazofanya Watanzania katika sekta ya Civil Societies kupaisha kazi zetu.

“Mfumo wa sera ya serikali iliyowezesha kuweka mkonga wa taifa wa kilomita zaidi ya 12,000 nchi nzima imetuwezesha kuunganisha shule 15 na serikali huduma ya kimtandao ya kasi.” alisema Nicholas.
Aliongeza kwa kusema msingi wa sera pia unatokana na ilani ya chama tawala ambapo ni Chama cha Mapinduzi (CCM ) kupitia ukurasa wake wa 98 wa ilani yake ya mwaka 2020 – 2025.

Nazar alimaliza kwa kusema malengo ya mradi ifikapo mwaka 2034 ni kuwa na Community Network Hubs 200 Tanzania nzima ili kuunganisha watu million 4 na mtandao wa kasi na kutoa elimu digiti kwa vijana na wanawake Wajasiriamali milioni 1.5.