The House of Favourite Newspapers

NEC Yamteua Catherine Ruge Kuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema

0
Catherine Nyakao Ruge.

Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbungewa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada yakupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.

Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:-

Kailima, R.K

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Leave A Reply