SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI, WAPO KAMILI KWA SIMBA DAY
Baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa nchini Afrika Kusini hatimaye wakijiandaa kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18, hatimaye kikosi cha Simba kimerejea salama jijini Dar.
Simba ambayo ilikuwa Sauzi kuweka kambi ikiwa na wachezaji wake wapya kasoro Haruna Niyonzima, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki katika Tamasha la Simba Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jumanne ijayo Agosti 8 dhidi ya Rayon Sports.
Wachezaji wa timu hiyo waliwasili kwa mafungu ambapo hali hiyo ilitokana na kupata tiketi katika ndege tofauti.
Katika tamasha hilo, Simba inatarajiwa kumtambulisha mchezaji wake mpya Haruna Niyonzima ambaye hakuwepo kambini kutokana na masuala ya kifamilia aliyokuwa akiyaweka sawa nchini Rwanda ambapo ni nyumbani kwao.
[…] cha Simba leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar ikiwa ni maandalizi […]