The House of Social Media
gunners X

Jini Mweusi 56

0

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinogewa na penzi la changudoa mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana huyo ungeweza kubadilisha kila kitu.

Je, nini kitafuatia?

SONGA NAYO…

Dickson akashtuka kutoka katika usingizi mzito, mwili wake ulikuwa umechoka mno, akaangalia huku na kule, alitaka kufahamu alikuwa sehemu gani kwani kwa jinsi kitanda kile kilivyokuwa, alikuwa na uhakika kwamba hapo hapakuwa nyumbani kwake.

Akayafikicha macho yake na kuiangalia sehemu hiyo, ilikuwa katika nyumba ya wageni. Kumbukumbu zake zikaanza kurudi nyuma ili ajue sababu zilizomfanya kuwa ndani ya chumba hicho.

Hapo ndipo alipokumbuka kwamba mara ya mwisho kabisa alikuwa chumbani na mwanamke, walishikana hapa na pale, kilichofuata, hakukikumbuka. Akaelekea katika suruali yake, alitaka kuona kama fedha zake zilikuwepo, hakukuta kitu, si fedha tu, hata simu yake pia haikuwepo.

Akajikuta akiuma meno kwa hasira, mwili ukaanza kumtetemeka mithili ya mtu anayesikia baridi, kwa sababu kwa mbali mwanga wa alfajiri ulishaanza kutokeza, akainuka, akavaa nguo zake na kuondoka chumbani hapo huku akiwa na kofia yake kichwani.

Hakumsalimia dada wa mapokezi, aliunganisha moja kwa moja mpaka nje, akalifuata gari lake na kuondoka huku akiwa na hasira kali dhidi ya changudoa aliyemlevya na kumuibia

Alichokitaka ni kulipa kisasi, hakutaka kumuacha changudoa huyo aendelee kuishi kwani akili yake ilimwambia kwamba kabla ya kuondoka, alimwangalia usoni na kumgundua alikuwa nani, hivyo akaenda kuwaambia marafiki zake.

Hakutaka kuona siri hiyo ikivuja, kwa hali na mali, tena kwa gharama yoyote ile ilikuwa ni lazima amuue changudoa huyo. Hakujua alifananaje, alichokikariri kutoka kwake ni miguu yake, ilikuwa imejaajaa huku kwa mbali akiwa na matege. Mbali na miguu hiyo, sura yake ilikuwa na chunusi nyingi zilizomfanya kumpendezesha sana na kumfanya avutie.

“Nitamtafuta, na nitamuua tu, si yeye, hadi marafiki zake wote ni lazima niwamalize wote kwa kuwa najua atakuwa amewaambia tu,” alisema Dickson huku akionekana kuwa mwingi wa hasira.

Alichokifanya mara baada ya kufika ofisini ni kuagiza usiku wa siku hiyo katika sehemu zote ambazo zilikuwa na machangudoa waliokuwa wakijiuza, ilikuwa ni lazima polisi waende kuwakamata na ikiwezekana wawaweke ndani na yeye mwenyewe kwenda kuwaangalia.

Polisi walishangaa sababu ya Kamanda Dickson kuamua hivyo lakini hakukuwa na mtu mwenye maswali, kwa kuwa amri ile ilitolewa na mkuu wao, ikawabidi waifuate kama walivyotakiwa.

Usiku wa usiku huo polisi wakafanya doria sehemu zote zilizokuwa na machangudoa, wengi wakakamatwa na kupelekwa vituoni, asubuhi iliyofuata Kamanda Dickson akaanza kutembelea kila kituo na kuwaangalia machangudoa hao, alipoona hakuna mbaya wake aliyekuwa akimtafuta, akaachana nao.

“Nitampata tu, ni suala la muda tu,” alijisemea Kamanda Dickson.

*     *     *

Kichwa cha Pamela kilikuwa na mawazo mengi, stori alizopewa kuhusu mtu mwenye gari nyeusi ambaye alikuwa akiwachukua wasichana na kwenda kuwaua ilimuogopesha.

Moyo wake ulijawa na hofu lakini hiyo haikuwa sababu iliyojitosheleza ya kumfanya asimame na kuachana na shughuli zake. Alitoka jijini Arusha mpaka Dar es Salaam kwa sababu alihitaji fedha, alijipanga na katika kipindi ambacho aliishi jijini Dar, tayari aliyaona mafanikio, hivyo kuachana na biashara ya kujiuza ilikuwa ngumu.

“Umakini ndiyo unaohitajika tu,” alijisemea.

Machangudoa wote wa Kinondoni hawakuwa watokaji, ili ufanye nao ngono ilikuwa ni lazima iwe hapohapo makaburini au ndani ya gari lako, ila si kuondoka katika eneo hilo na kwenda hotelini au sehemu nyingine.

Kwa Pamela ilikuwa tofauti, aliyatoa maisha yake sadaka, alijua kwamba wanaume wengi hawakupenda kufanya ngono makaburini kwa kisingizio cha kuogopa laana, hivyo kama na yeye angefanya kama watu wengine basi asingepata fedha, hivyo ilikuwa ni lazima kufanya kama zamani.

Machangudoa wengine walimshangaa Pamela lakini hakuonekana kujali, alihitaji kuwa na fedha, hivyo hata suala la kuuawa, aliliita ajali kazini.

Siku ya kwanza ikapita, ya pili, ya tatu mpaka wiki nzima, hali ilikuwa ni amani tele, hakuuawa wala kukutana na mtu mbaya, wote waliokuja kwake ambao walimtaka kwenda kulala naye, walikuwa watu wema mpaka kufikia hatua akahisi kwamba inawezekana stori hizo zilikuwa ni uzushi tu.

Baada ya wiki nzima kukatika, hapo ndipo akajikuta mikononi mwa polisi. Hakuwa yeye, walikuwa na machangudoa wengine wengi, walifungwa pingu na kupelekwa vituoni.

Kila mmoja alishangaa, hakukuwa na taarifa kama siku nyingine ambapo kabla ya polisi kufanya doria, waliletewa taarifa, doria ya siku hiyo ilikuwa ya ghafla sana hivyo machangudoa wengi kujikuta wakiingia mkenge.

Alilala sero na wenzake, kesho yake, hawakuachiwa bali waliambiwa wasubiri kwani Kamanda Dickson, mtu mwenye sura mbaya alikuwa akipita katika vituo vyote kwa ajili ya kuangalia idadi ya machangudoa hao kujua kama kuna muharifu aliyekuwa akimtafuta.

Je, nini kitafuatia? Usikose riwaya hii ya kusisimua Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply