The House of Social Media
gunners X

Mama, Baba Lishe Saccos kuzinduliwa Dar

0

1Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama Lishe na Baba Lishe, Ramadhan Mohanzu, Mshauri wa Jumuiya hiyo, Said Mohamed, Katibu wa Soko la Machinga Dar, Agatha C. Kiluhumo na Katibu wa Soko la Ilala.

2.Wanahabari wakichukua matukio.Wanahabari wakichukua matukio.

3.Mshauri wa Jumuiya hiyo, Said Mohamed (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Mshauri wa jumuiya hiyo, Said Mohamed (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).

4.Viongozi wa Jumuiya hayo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.Viongozi wa jumuiya hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

JUMUIYA ya Mama Lishe na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, wamepanga kuzindua mfumo mpya wa ‘Mama na Baba Lishe Saccoss’ kwa lengo la kuwawezesha katika masuala ya huduma za kifedha, namna ya kutafuta ufumbuzi na kutatua baadhi ya matatizo na kupata mahitaji mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe, Ramadhan Mohonzu amesema kutokana na mama na baba lishe kuwa wengi maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, manispaa nyingi hapa Tanzania zimeamua kutafuta ufumbuzi kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha vikundi vya mikopo kama vile Saccoss.
Mhonzu amesema Mama na Baba Lishe wanakumbwa na matatizo ya kukosekana kwa mitaji inayosababisha wengi wao kukosa mikopo hivyo wameamua kutatua matatizo yao kwa kuanzisha Saccos.

Hata hivyo, amesema wanaamini Saccos hiyo itaweza kusaidia na kuratibu maendeleo yao wakiwa na uongozi bora juu ya watoa huduma za vyakula kwa watu wa nyanja zote.
Naye mshauri wa jumuiya hiyo, Saidi Mohamed amesema mfumo huo utawezesha kutambulika na kukuza jamiii kwa jumuiya ya baba na mama lishe, ambapo watatambulika katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Mohamed amesema, Saccos hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 15, mwaka huu ambapo itawakutanisha mama na baba lishe kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Ukumbi wa PTA- Sabasaba).

Naye katibu wa mama lishe katika soko la Ilala, Jane Nyanda amesema wamekuwa na changamoto nyingi za muda mrefu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ambao umekuwa sanjari na kushuka kiuchumi katika biashara zao na kuongeza kuwa Saccos hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kimapato.
NA DENIS MTIMA /GPL

Leave A Reply