Avril na kolabo kali Bongo
Mwimbaji machachari kutoka Kenya, Avril Nyambura ‘Avril’.
Mwimbaji machachari kutoka Kenya, Avril Nyambura ‘Avril’ ambaye ni maarufu Bongo kupita nyimbo kadhaa kama vile, Nimekuja Chokoza na Hello Baby aliomshirikisha mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz anatajwa kuwa ni mmoja wa wasanii wa kike wenye bahati zao baada ya kufanya kolabo kali na mastaa wa Kibongo na kujiweka vizuri kwenye tasnia hiyo hapa nchini.
Mpaka sasa Avril amefanya kolabo na wasanii kama Ambwene Yessaya ‘AY’ liyemshirikisha katika wimbo wake wa Leo Remix kabla ya baadaye naye kumshirikisha katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la No Stress.
Mbali na AY, Avril amefanya ngoma inayokwenda kwa jina la Hello Baby na mkali wa Nai Nai, Ommy Dimpoz na kushirikishwa na mwanamuziki Ben Pol kwenye wimbo unaokwenda kwa jina la Ningefanyaje.
Kabla ya kolabo hizo ikumbukwe kuwa wanadada huyo ameshawahi kutokelezea kwenye Video ya Kesho ya Nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akiwa kama video queen wa kichupa hicho.

