The House of Social Media
gunners X

Kilichonitokea Baada ya Kubakwa na Kaka Yangu-23

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Dorcas aliposema kwamba kaka yake Evance aliendelea kumfundisha masomo na namna ya kutumia laptop yake ambapo alimweleza ilikuwa muhimu kufahamu kuitumia lakini siku moja alifanya kitu kilichomshangaza sana.

Je, ni kitu gani hicho?

Songa mbele na mkasa huu wa kuhuzunisha…

Siku hiyo akiwa ananifundisha alifungua picha za watu waliokuwa wakifanya mapenzi, alipobaini nimeziona aliniambia nisijali kwani kwenye kompyuta kuna mambo mengi na kwa kuwa nilikuwa mkubwa ninapojisikia niwe naziangalia kwa lengo la kujifunza mambo ya mapenzi.

Licha ya kutopendezwa na kitendo kile sikutaka kumuonesha kwamba nilichukia, nilimwambia sawa lakini moyoni niliapa kutofanya hivyo.

Tangu siku hiyo kila alipokuwa akinifundisha akawa anafungua zile picha za wanaume waliokuwa utupu au kukumbatiana na wasichana ndipo nikagundua hakuwa na nia njema. Siku moja pale nyumbani waliondoka wote nikabaki peke yangu, nilipomaliza kupika kaka alirejea na mfuko wa rambo akaniita sebuleni kisha kunikabidhi na kuniambia aliniletea zawadi nzuri sana.

Niliupokea mfuko huo na kumuuliza ni zawadi gani aliyoniletea, akacheka na kuniambia ni zawadi ya kawaida ila anaamini nitaipenda, nilimshukuru nikauweka ule mfuko juu ya meza ndogo iliyokuwa pembeni ya sofa.

Baada ya kuuweka pale, kaka aliniambia hapakuwa sehemu sahihi na kuniomba niende nayo chumbani kwangu kisha nikaiangalie zawadi hiyo.

Alipotoa kauli hiyo, nilimwambia kwa kuwa aliniletea zawadi asiwe na shaka nitaiangalia kwa wakati wangu lakini alisisitiza niende nikaiangalie chumbani kwangu muda ule.

Kuepusha kuona sikumheshimu niliuchukua ule mfuko na kwenda nao chumbani kwangu lakini sijui kwa nini sikuwa na haraka ya kutaka kujua ni zawadi gani kaka aliniletea, niliuweka ule mfuko kitandani nikatoka.

Nilipofika sebuleni kaka alitabasamu na kuniuliza kama nilipenda zawadi aliyoniletea, nikamwambia nimeuweka tu mfuko kitandani bila kuiangalia.

Aliniuliza kama sikufurahi yeye kuniletea zawadi, nikamwambia nilifurahia lakini kwa kuwa ilikuwa yangu ningeiangalia muda wowote nitakaopenda.

Baada ya kumwambia hivyo, ghafla alipoteza uchangamfu nigagundua nilimkwaza nikamuuliza kwa nini alipenda niiangalie ile zawadi muda ule!

Nilipomwambia hivyo alisema hakuamini kama ningemfanyia vile kwa sababu kawaida ya mtu yeyote anapoletewa zawadi huwa na shauku ya kuiona lakini mimi sikufanya hivyo.

Kumtoa shaka nilimwambia aondoe shaka nitaiangalia na kumshukuru tena kwa kuniletea zawadi hiyo, yaani nashindwa kuelewa kwa nini sikuwa na shauku ya kuiangalia.

Kufuatia kumweleza hivyo, kaka alibaki akiniangalia kisha alinieleza kwamba nitakapoiangalia nimwambie kama niliipenda, nikamwambia asiwe na shaka ndipo akawasha TV akaanza kuangalia.

Wakati kaka akiangalia runinga, nikiwa nimeketi kwenye sofa ambalo lilikuwa kushoto kwake nikawa najiuliza ni zawadi gani aliyoniletea aliyokuwa akinilazimisha kuiangalia.
Baada ya kujiuliza niliamka na kwenda chumbani kwangu nikaufungua ule mfuko, nikakuta ndani kuna kitu kama nguo kikiwa kimefungwa kwenye mfuko wa khaki nikaufungua.

Nilishangaa kuona kuna chupi tatu nzuri sana za rangi nyeupe, maziwa na pinki pia kulikuwa na vitambaa vyeupe vinne, nikajiuliza kaka kuniletea zawadi ya aina ile alikuwa na maana gani.

Ukweli nguo hizo za ndani zilikuwa nzuri sana tofauti na nilizokuwanazo lakini bado nilijiuliza kwa nini kaka yangu aniletee nguo hizo nyeti, nikazirudisha kwenye mfuko kisha nikauweka ndani ya begi langu.

Niliamua kuziweka kwenye begi kuhofia kama mama angeziona angeniuliza nilizitoa wapi, hata kama ningemwambia nililetewa na kaka asingenielewa na kuniambia kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea baina yetu.

Baada ya kuziweka nilikwenda sebuleni na kumkuta kaka akiangalia runinga, alipogeuka na kuniona alijua nilikwenda kuangalia zawadi aliyoniletea, akaniuliza kama niliipenda zawadi hiyo.

Kufuatia kuniuliza hivyo, nilimuuliza akiwa kama kaka yangu kwa nini aliamua kuninunulia nguo za ndani badala ya kuniletea zawadi nyingine kama madaftari nk.
Kaka alicheka na kunieleza hakukuwa na ubaya kwa kaka kumnunulia dada yake nguo nzuri za ndani ili apendeze, nikamwambia alikosea sana hivyo nitamkabidhi zawadi zake.

Nilipomwambia hivyo, aliniambia niache ushamba kwani hakukuwa na ubaya wa kaka kumnunulia nguo za ndani dada yake kuonesha anavyompenda na kumjali.

Wakati tunaendelea na mazungumzo, mama alifika hivyo tulibadili maongezi ndipo mama alituuliza kuhusu habari za pale nyumbani tukamwambia zilikuwa nzuri sana.
Hata hivyo, mama aliyeonekana kuwa na haraka alituambia alifuata hela ambapo aliingia chumbani kwake hakukaa sana akatuaga kwamba anakwenda kumuona mtu mmoja.

Baada ya mama kuondoka, kaka aliendelea kuniambia kwamba alinishangaa sana badala ya kumshukuru kwa zawadi nzuri aliyoniletea nilimshambulia kwamba alikosea.
Kwa kuwa sikuwa na amani moyoni juu ya zawadi alizoniletea, nilimwambia asubiri niende nikamchukulie zawadi zake ili akampatie mtu mwingine.

Alipoona nataka kuinuka alinizuia na kuniomba msamaha ambapo alisema kama sikupendezwa na zawadi nizipokee tu na kwamba siku nyingine hataniletea zawadi za aina hiyo.

Kufuatia kuniomba msamaha niligundua alielewa kwamba sikufurahishwa na zawadi zake na kwa kumheshimu nilimwambia yalikwisha na kuahidi kuzitumia.
Je, kilifuatia nini? Usikose wiki ijayo. Maoni, nicheki kupitia namba hiyo hapo juu.

Leave A Reply