The House of Social Media
gunners X

John Woka ‘chapombe’ aliyetingisha Bongo Fleva

0

c1c729aa6d5ac3453162287f7735eee1Michael Muhina ‘John Woka’.

Ni vigumu kuamini kama kuna wakati msanii huyu aliyewafanya mashabiki kuvunjika mbavu wakisikiliza kazi zake UNAWEZA kupata taabu kidogo kumtafuta na kumfahamu kijana mwenye jina la Michael Muhina, lakini utampata haraka kama utamtafuta kwa jina la John Woka, msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyejipatia umaarufu mkubwa miaka ya 2000.

Kilichompatia umaarufu huo ni kitendo chake cha kuimba huku akiigiza sauti ya kilevi, lakini iliyokuwa ikitoa maneno yenye mantiki, kiasi cha kujikusanyia mamia ya mashabiki kila alipokwenda katika shoo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

John Woka alifanya kazi na wasanii wengi wakiwemo Wagosi wa Kaya, lakini zaidi alikuwa ni mshirika mkubwa wa msanii mwingine wa reggae, Gerald Simba aliyefahamika zaidi kama Ras Lion.

Moja kati ya kazi maarufu zaidi aliyofanya na Ras Lion ni kibao kilichotingisha sana, kilichosema Hii Kitu ambacho mashabiki walikipokea vizuri na kilipata ‘airtime’ ya kutosha katika vituo vingi vya redio enzi hizo.

Aliwahi pia kufanya kazi na Keisha iitwayo Nikikupata na pia akiwa na Ras Lion, walimshirikisha mkongwe Mike T katika ngoma iliyoitwa Bitozi. Kazi nyingine aliyofanya na swahiba wake huyo mkubwa kimuziki iliitwa Yalaa, Hodi Mganga na ile ambayo nayo ilisumbua sana, iliyojulikana kama Umasikini Huu.

Kwa jinsi John Woka alivyokuwa ‘aki-flow’ katika muziki wake, ilikuw wa kweli, kwani hata katika baadhi ya video za nyimbo hizo, msanii huyo aliipatia vizuri nafasi yake ya
uigizaji wa kilevi, kama ambavyo mwigizaji maarufu wa vichekesho, Masele navyofanya.

ata hivyo, aina ya muziki aliokuwa akiufanya, ilionekana kukosa soko mbele ya mashabiki na wakati fulani, aliwahi kukiri hali hiyo, akilaumu kuwa wapenzi wa muziki wa Kitanzania wanapenda zaidi kusikiliza nyimbo za mapenzi na zenye midundo ya kuchezeka, badala ya tungo zenye mafunzo.

Hali hiyo, ndiyo iliyochangia kwa kiwango kikubwa kuanza kupotea kwake jukwaani, kwani pia aliwahi kusema kuwa mashabiki wake wengi walimshauri ni bora angejiingiza katika komedi kuliko kuendelea na aina hiyo ya muziki, kitu ambacho alikubali na kuanza kushughulika kwenye fani hiyo.

Katika kipindi ambacho mashabiki wanapenda zaidi muziki wa kizazi kipya naowafanya wajirushe kwa shangwe jukwaani na kwenye kumbi, ni wazi kuwa John Woka atalazimika kufanya ubunifu upya, kama lengo lake ni kurejea makali yake ya miaka hiyo.

Vinginevyo ni vigumu kuamini kama kuna wakati msanii huyu aliyewafanya mashabiki kuvunjika mbavu wakisikiliza kazi zake, atarudi tena kuwapa burudani kama alivyowahi kufanya huko nyuma. Aina ya muziki wake, ulifanana kwa kiwango kikubwa na ule wa vijana kutoka Tanga, Wagosi wa Kaya.

Ndiyo maana, katika kizazi cha sasa cha wasanii wanaotaka muziki wao kufanana na ule wa Nigeria au Marekani, John Woka na kaka zake Wagosi wa Kaya, wanapaswa kukaa chini upya na kuangalia kama wanaweza wakatokaje ili kuendelea na jukumu la kuelimisha, kuburudisha na kufundisha jamii kupitia muziki!

Leave A Reply