
Jay Z.
New York, Marekani
MAUZO ya albamu za wasanii kwa kiasi kikubwa yameshuka kutokana na kukua kwa teknolojia. Nyimbo nyingi zimekuwa zikifika kwa mashabiki mapema, ambapo ni tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, hiyo imesababisha hata soko la fani hiyo nalo libadilike pia.
Marapa 50 Cent na Kanye West waliwahi kuingia kwenye ushindani wa kibiashara na kutengeneza bifu ambayo iliwasaidia kuuza nakala nyingi za albamu zao mwaka 2008, lakini leo hii hali ni tofauti na wanatafuta kuingiza fedha kupitia kitu kingine na siyo kutegemea albamu.
Kanye West.
Wasanii wengi wamekuwa wakiingiza fedha nyingi kupitia shoo. Malipo hayo pia yanatofautiana kutokana na sehemu na wakati, miezi kadhaa iliyopita kampuni inayohusika na uwakala wa shoo za wasanii ilitoa orodha ya kiasi wanacholipwa wasanii wa Hip Hop kwa shoo moja hasa ndani ya Marekani na nchi za jirani. Alama ya + inamaanisha kiwangi husika kinaweza kuwa zaidi ya kilichotajwa:
A$AP Ferg
Dola 25,000
(Sh milioni 53)
Bow Wow
Dola 25,000
(Sh milioni 53)
Earl Sweatshirt
Dola 25,000
(Sh milioni 53)
De La Soul
Dola 40,000
(Sh milioni 84)
Busta Rhymes
Dola 40,000
(Sh milioni 84)
The Game
Dola 40,000-50,000
(Sh milioni 84-105)
Big Boi
Dola 50,000
(Sh milioni 105)
Soulja Boy
Dola 50,000+
(Sh milioni 105)
Juicy J
Dola 60,000
(Sh milioni 126)
Nelly
Dola 65,000
(Sh milioni 136)
Lupe Fiasco
Dola 65,000-70,000
(Sh milioni 136-147)
Wale
Dola 70,000
(Sh milioni 147)
B.o.B
Dola 70,000
(Sh milioni 147)
Jeezy
Dola 70,000
(Sh milioni 147)
Big Sean
Dola 75,000
(Sh milioni 157)
Common
Dola 75,000
(Sh milioni 157)
Mac Miller
Dola 75,000
(Sh milioni 157)
Ludacris
Dola 80,000+
(Sh milioni 168)
2 Chainz
Dola 85,000
(Sh milioni 178)
Childish Gambino
Dola 85,000
(Sh milioni 178)
A$AP Rocky
Dola 90,000-120,000
(Sh milioni 189-252)
Rick Ross
Dola 100,000
(Sh milioni 210)
Lauryn Hill
Dola 100,000
(Sh milioni 210)
Snoop Dogg
Dola 100,000
(Sh milioni 210)
The Roots
Dola 100,000+
(Sh milioni 210)
Kid Cudi
Dola 110,000+
(Sh milioni 231)
Wiz Khalifa
Dola 115,000
(Sh milioni 241)
J. Cole
Dola 125,000
(Sh milioni 262)
Kendrick Lamar
Dola 125,000+
(Sh milioni 262)
50 Cent
Dola 150,000+
(Sh milioni 315)
Dau lake lilikuwa juu zaidi ya hili lakini lilishuka kutokana na kushuka kimuziki pia huku nguvu kubwa akielekeza kwenye kuigiza filamu.
Nicki Minaj
Dola 250,000+
(Sh milioni 525)
Dau litakuwa limepanda zaidi ya hapo kwa kuwa jina lake bado ni kubwa na nyimbo zake zinafanya vizuri kwenye chati mbalimbali.
Lil Wayne
Dola 300,000+
(Sh milioni 630)
Huyu ni kama ilivyo kwa Nicki, jina lake bado ni kubwa na anaendelea kusikika kwenye chati za muziki, dau lake pia linaweza kuongezeka kila mara.
Drake
Dola 350,000-600,000
(Sh milioni 735-bilioni 1.3)
Uzuri wake ni kuwa anajituma na anabadilika katika staili mbalimbali, dau lake linapanda kila wiki.
Macklemore
Dola 350,000-700,000
(Sh milioni 735-bilioni 1.3)
Siyo maarufu kama wenzake kwa kuwa ni Mzungu na ni Wazungu wachache wanaoweza kutamba kwenye Hip Hop, lakini bado shoo zake ni za bei kubwa.
Kanye West
Dola 500,000+
(Sh bilioni 1)
Mume wa Kim Kardashian anaendelea kuiteka dunia kutokana na umaarufu wa yeye na mkewe huku urafiki wake na Jay Z ukimuongezea umaarufu.
Jay Z
Dola 1,000,000+
(Sh bilioni 2.1)
Huyu jamaa anajua kujiheshimu, huwezi kumsikia kwenye skendo zisizo na kichwa wala miguu, anajiheshimu na ameshajiweka kwenye levo flani ambayo hauwezi kumshusha. Ndoa yake na mkewe, Beyonce, kudumu muda mrefu kumemuongezea sifa ya kuwa mume mtulivu na rapa bora.
no eminem no snoopy why