×

Ali Chocky atupiwa vyombo nje

chockyMwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Ali Chocky.

Gladness mallya
MWANAMUZIKI wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Ali Chocky ametolewa vyombo nje na mabaunsa baada ya kupangishwa nyumba yenye kesi, Risasi Jumamosi linahabarisha.

Kikizungumza chanzo makini kilisema kwamba Chocky na familia yake walikuwa wamepanga nyumba maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alilipa kodi ya miezi nane kwa kila mwezi akilipa shilingi laki nne ambazo jumla alitoa milioni tatu na laki mbili.

Baada ya kulipa fedha hizo alihamia kwenye nyumba hiyo na kukaa mwezi mmoja na nusu pasipokujua kwamba nyumba hiyo ina kesi mahakamani, hivi karibuni alitolewa nje na vyombo vyake huku mabaunsa wakiwa ndiyo watekelezaji wa zoezi hilo.

Paparazi wetu alimtafuta Chocky ambaye alikiri kupatwa na tukio hilo na kusema ameumia kwani amepata hasara kutokana na fedha alizokuwa ameshazilipia.

“Ni kweli nilitolewa vyombo nje na familia yangu nikiwa nimeshalipa kodi ya miezi nane bila kujua nyumba hiyo ilikuwa na kesi na tulikaa kwa mwezi mmoja na nusu tu, ni kama yule aliyenipangisha aliniingiza mkenge nitafuatilia kisheria kuona kama naweza kupata haki yangu, kwa sasa tumehifadhiwa kwa ndugu maeneo ya Mburahati,” alisema Chocky.

Leave a Comment