×

‘Baba mzazi ananitaka kimapenzi’

IMG-20151205-WA0001

Binti huyo akiwa amekaa kwenye kiti.

Dustan Shekidele, Moro

Fedheha! Binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa kimaadili) Amelia kuwa baba yake mzazi wa kumzaa ambaye ni mfanyabiashara maarufu mjini hapa aliyetajwa kwa jina moja la Ima, amekuwa akimtaka kimapenzi hivyo kuwekewa mtego gesti na kuuvaa mzimamzima.

Tukio hilo la aibu lilijiri wiki iliyopita kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) ya Midway iliyopo maeneo ya Msamvu mjini hapa ambapo kabla ya tukio, binti huyo aliilalamikia Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na kwamba tayari alikuwa amemuwekea mtego mzazi wake huyo kwa maelekezo ya wajomba zake waliotaka ushahidi wa jambo hilo.

IMG_20151211_203918

Gesti iliyokuwa itumike kwenye sakata hilo.

Dakika chache baada ya kujiri kwa tukio hilo, OFM ilifika kwenye gesti hiyo na kukuta umati uliokuwa umefunga mtaa kutaka kujua kulikoni baba mzazi kufumwa gesti na binti yake wa kumzaa.

Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni mjomba wa binti huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Massawe alikuwa na haya ya kusema:
”Ima ni shemeji yangu aliyemuoa marehemu dada yangu. Baada ya dada yangu kufariki dunia, cha ajabu amekuwa akimtongoza binti yake wa kumzaa. Amekuwa akimsumbua kila siku akimtaka kimapenzi.

“Awali tulijua mwanaye anamsingizia hivyo tuliamua kushirikiana na binti huyo tukamwekea mtego ambao kweli leo umefyatua, amekutwa laivu akiwa chumbani tena gesti na binti yake.”

Kwa upande wake, binti huyo alipohojiwa na gazeti hili alisema baada ya mama yake kufariki dunia miaka kadhaa iliyopita na yeye kumaliza shule ya msingi, baba yake huyo anayeishi naye amekuwa akimsumbua kila siku akimtaka kimapenzi jambo ambalo limekuwa likimsumbua kiasi cha kumkumbuka mama yake.

”Mwanzoni nilihisi labda ni upendo wa baba tu kwa mwanaye lakini ghafla baba yangu mzazi alianza kunisumbua akinitaka kimapenzi, nikimuomba fedha ya matumizi ananiambia tufanye kwanza mapenzi.

“Nimekuwa nikimkatalia lakini hivi karibuni amezidisha kasi ndiyo maana nikaona niwaambie wajomba ambao waliniambia nimkubalie wamwekee mtego na kweli leo alikuja kunichukua nyumbani na gari lake akanileta hapa gesti akitaka nimpe penzi.

“Baada ya kuingia chumbani, kabla hajanivamia nikawajulisha wajomba niliokuwa nawasiliana nao ambao walifika na polisi na kumkuta baba akijiandaa kufanya mapenzi na mimi ambaye ni binti yake kabisa wa kumzaa,” alisema binti huyo.

Baada ya kumnasa, wajomba hao, wakishirikiana na polisi walimpeleka shemeji yao huyo kwenye Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa ambapo suala lake linashughulikiwa kwenye Dawati la Jinsia.

Kabla ya kwenda mitamboni gazeti hili liliwasiliana na jamaa huyo ili kujua analizungumziaje tukio hilo baada ya kuachiwa huru ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Nitakupigia uje ofisini kwangu tuongee.”

Leave a Comment