Mshinda wa Shindano la Miss Universe 2015, Pia Alonzo Wurtzbach.
MSHINDI wa Shindano la Miss Universe 2015, Pia Alonzo Wurtzbach kwa mara ya kwanza amefungukia watu wanaomponda Miss Colombia kuwa waache mara moja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Miss Pia aliongelea kuhusiana na mshiriki huyo wa Colombia ambaye alitaka kupewa taji kimakosa baada ya kutajwa kama mshindi kimakosa na mshereheshaji (MC), Steve Harvey katika fainali zilizofanyika hivi karibuni.
“Hii ni kwa ajili ya mashabiki zangu ambao bado mnaendelea kunipigania… tafadhalini acheni kumzonga Miss Colombia. Uongozi wa Miss Universe lengo lao ni kuwaunganisha wanawake wote duniani na kuwawezesha kupitia shindano hili.
“Miss Colombia ni mwanamke wa maajabu, bado niko naye milele kwa sababu ni mtu adimu. Kwa wiki tatu tulikuwa pamoja, nilimuona ni kwa jinsi gani alivyo shupavu, mrembo ndani na nje,” aliandika Pia.