×

Mumeo aende masaji wakati ujuzi unao?

couple-happy-in-bed-comp-680x380SHANGINGI leo niwape hi, nimejisikia kuchanganya na kizungu kidogo kwa sababu mada inahitaji hivyo, si unajua mambo ya masaji hayo ni ya wenzetu, zamani usingesikia bibi kaenda jumba la masaji!

Mada itawafundisha jinsi ya kumlea mume pale anapolalamikia maumivu ya mwili; wanawake tumekuwa na tabia kwamba mumeo akikwambia anajisikia vibaya, unakimbilia kumwambia aende hospitali au unakwenda kumnunulia panadol apunguze maumivu…tunakosea kabisa.

Daktari, nesi au tabibu ni wewe mwenyewe shoga yangu, hebu nikupe siri moja, usiniulize mchaichai nitaupata wapi, kwani uko mwingi sokoni na kwenye maduka ya asili, chukua nazi zako mwanamke mwenzangu, zikune halafu chuja taratibu mpaka upate tui zito, lichemshe ili upate mafuta ya nazi, ule muda ambao tui lako liko jikoni chukua majani ya mchaichai changanya kwenye tui hilo.

Wakati linachemka changanya na mdalasini pamoja na hiliki, acha tui lichemke mpaka ligande, likishaganda unatoa mafuta mazuri yanayonukia kisha chuja na uweke kwenye chupa safi.

Muinue mumeo kamuogeshe, ikiwezekana hata kumbeba, mbebekwani huwezi kushindwa kufanya hivyo, mbona mkiwa kwenye mahaba uzito huuoni? Kamuogeshe na baada ya kumkausha maji chukua mafuta yako umpake mwili mzima, kisha fanya masaji taratibu, baadhi ya wanawake wanawapeleka waume zao kwenye masaji, hivi kwa nini mumeo akashikweshikwe na mwanamke mwenzako wakati wewe upo?

Shoga’angu mpapase taratibu mumeo huku unamfanyia masaji, hakikisha kila idara unaifikia, utakapofika katika mji mkuu wa mumeo sidhani kama maumivu yatakuwepo, lazima atataka chakula cha usiku, mpe shoga yangu kwa raha zenu! Tukutane tena wiki ijayo.

Leave a Comment