Wiz Kid akizungumza kabla ya kugawa zawadi ya pesa kwa mashabiki
Kijana aliyepanda jukwaani kuimba nyimbo za Wizzy.
STAA wa Ngoma ya Ojuelegba kutoka Nigeria, Wizkid jana Desemba 29, ametoa zawadi ya pesa taslim Naira milioni 1 (sawa na Tsh. mil 10.9) kwa mashabiki wake alifanya shoo yake ya nguvu ya Industry Night kwenye Ukumbi ujulikanao kama Oriental Hotel huko Lagos Nigeria. Shoo iliyojaza na kuwavutia mashabiki kwa aina yake.
Kijana akiimba moja ya nyimbo za Wizzy
Siku chache kabla ya shoo hiyo, Wizzy alitangaza kutoa zawadi ya pesa N250,000 kwa kila shabiki atakaeimba nyimbo zake kwa ufasaha. Ni mashabiki wanne walioweza kupata zawadi hizo.
Wizzy akionesha kiktita kabla ya kumkabidhi mshindi.
Wizzy aliwauliza mashabiki kama kuna yeyote angeweza kuimba wimbo wake wakati ‘sound track’ ikipigwa chini kwa chini.

Shabiki wa kwanza alipanda jukwaani na kuanza kutumbuiza nyimbo za Wizzy bila kukosea msitari hata mmoja, mashabiki waliokuwa wakimsikiliza walilipuka kwa shangwe kuonesha kukubali kipaji cha shabiki aliyekuwa aikiimba hivyo kupendekeza awe wa kwanza kujipatia N250,000 kutoka kwa Wizzy.
Kitita kabla ya kuwapa washindi.”Napenda kusema nashukuru kuimba wimbo wangu bila kukosea, inaonesha mnavyoikubali kazi yangu”, Wizkid alisema na kumpa kijana N250,000.
Shabiki aliyekuwa amechorwa kifuani tatuu ya sura ya Wizzy.
Shabiki mwingine ni aliibuka jukwaani, japo hakuweza kuimba wimbo hata mmoja wa Wizzy lakini alipovua shati lake, kifua kilionesha amechorwa tatuu kubwa inayoonesha sura ya Wizzy.
Mashabiki walikubali azawadiwe na yeye N250,000 hivyo Wizzy akampa kama mashabiki walivyopendekeza.
Mmoja ya wadada wawili waliojipatia zawadi ya N250,000 kila mmoja kutoka kwa Wizzy.

Washindi wengine wawili ni waichana waliokuwa wameremba kucha zao, nao walipatiwa N250,000.