×

Mazishi ya Abel yawatoa machozi mamia waliohudhuria

IMG_1089

Mwili wa kijana Mtanzania, Abel Machanga, mkazi wa Mombasa-Ukonga aliyefariki dunia akipatiwa matibabu nchini India ukiwa kanisani.

IMG_1095

Wazazi wa Abel wakifatilia kanisani wakati wa Misa.IMG_1101

Ukiwa kanisani.IMG_1123Mwili wa marehemu ukipakizwa katika gari.

IMG_1069

MWILI wa kijana Mtanzania, Abel Machanga, mkazi wa Mombasa-Ukonga aliyefariki dunia akipatiwa matibabu nchini India, umezikwa jana Februari, katika makaburi ya Kanisa Katoliki huko Pugu, Dar, baada ya kukaa zaidi ya siku 31 toka alipoaga dunia.
Mazishi hayo yalifanyika katika mazingira ya huzuni na vilio kwa watu wengi waliohudhuria tukio hilo. Kutokana na mwili wa marehemu kukaa muda mrefu na kuanza kuharibika, ilikuwa ni vigumu kwa watu wengine kuruhusiwa kuuaga, ambapo ni ndugu tu waliopewa dakika chache kuuaga mwili huo, jambo ambalo lilizidisha vilio kwa ndugu hao.
Kabla ya hapo marehemu alifanyiwa ibada ya kumwuombea katika Kanisa la KKT lililopo Madafu, Mombasa.
Marehemu Abel Machanga amezaliwa Februari 7, 1991 katika kijiji kilichopo Nzega mkoani Tabora, akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watano wa Mzee Machanga. Alisoma elimu ya msingi Shule ya Bunge, Dar, mwaka 1998 hadi 2004 na kupata elimu ya sekondari katika shule ya Migrend jijini Dar mwaka 2005 hadi 2008.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alisomea masuala ya computa katika chuo cha Computa cha VCC mwaka 2009 kisha akajiunga na chuo cha elimu ya biashara (CBE) mwaka 2011 hadi 2012 na kupata cheti kabla ya kusomea ufundi chuo cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam kuhusu umeme na magari ambapo aliitimu mwaka 2014.
Marehemu Abel alianza kuugua ugonjwa wa macho toka mwaka 2014 na kuanzishiwa matibabu katika hospitali ya CCBRT na baada ya muda alifanyiwa vipimo na kubaini ana uvimbe juu ya ubongo wa mbele. Katika kumpima, madaktari walimfanyia wa kansa, lakini hawakubaini chochote ambapo baada ya muda macho yake yalivimba na kutoka nje na kumsababishia kushindwa kuona kabisa.
Novemba 25 mwaka jana, alipelekwa India kwa matibabu zaidi ambako alifanyiwa oparesheni na kufanikiwa kumtoa robo tatu ya uvimbe, lakini cha kushangaza alianza kuonesha mabadiliko zaidi na kutokwa na damu nyingi mdomoni na puani na kuwekewa kipimo cha kupumuliwa lakini haikuweza kusaidia hadi alipofariki Novemba 31 mwaka jana.

Leave a Comment