×

Mambo iko Dar Live Valentine Day

Studio shot of young couple smiling and looking at each other

Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
NDANI ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live kutadondoshwa shoo baab kubwa ya Valentine Day Bash kwa ajili ya siku maalum ya wapendanao maarufu kama Valentine Day, Februari 14, mwaka huu.
Kama kawaida huwa si shoo za kitoto, bendi kongwe na maarufu nchini zitakuwepo kukonga nyoyo za mashabiki mbalimbali wa muziki zikiongozwa na Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Sikinde na TOT Taarab chini ya Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Kopa.

15825youngcoupleinlove1920x1200photographywallpaper.jpg
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo amewataka wakazi wa Jiji la Dar na viunga vyake kutopoteza bahati hiyo kwa kujumuika kwa pamoja katika shoo hiyo kwa ajili ya kukamilisha furaha ya sikukuu kwa wapendwa wao.

“Kawaida yetu ni kufurahisha na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki, hii ni fursa na nafasi pekee kwa ajili ya kuipendezesha sikukuu ya wapendanao, tumeandaa Valentine Day Bash itakayokuwa na bendi zilizoshiba kwa ajili ya kutoa ladha na kukata kiu za wapenda burudani,” alisema Mbizo.
Shoo hiyo itakayokuwa na kiingilio cha Sh 10,000 kwa kawaida na Sh 20,000 kwa V.I.P, itasindikizwa na burudani za watoto zitakazoanza asubuhi kwa kiingilio cha Sh 2,000 na kumalizika jioni kabla ya bendi zenye heshima nchini kuanza kuporomosha burudani mpaka kuchwee.

Leave a Comment