×

Chelsea hoi kwa PSG

cavani

Edinson Cavani (kulia) akishangilia pamoja na David Luiz baada ya kuifungia timu yake ya Paris Saint-Germain bao la pili dakika ya 78.

chelsea

Chelsea wakiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Paris Saint-Germain.

mikel

John Obi Mikel akiwatoka wachezaji wa Paris Saint-Germain.

Kikosi cha Chelsea usiku wa kuamkia leo kimeshindwa kufurukuta baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Paris Saint-Germain kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) hatua ya 16 Bora.

Wafungaji wa Paris Saint-Germain katika mechi hiyo walikuwa Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani huku bao pekee la Chelsea likifungwa na John Obi Mikel.

Mechi nyingine ya ligi hiyo ilikuwa kati ya Benfica na Zenit St Petersburg ambapo Benfica waliibuka kidedea kwa bao 1-0 lililofungwa na Jonas dakika ya 90.

Vikosi
PSG:
Trapp; Marquinhos (Van der Wiel), Thiago Silva, David Luiz, Maxwell; Matuidi, Thiago Motta, Verratti (Rabiot); Di María, Ibrahimović, Cavani.

Chelsea: Courtois; Azpilicueta, Ivanović, Cahill, Rahman; Fàbregas, Mikel; Hazard, Willian, Pedro; Costa.

Leave a Comment