×

Nilivyoivunja Ndoa Yangu na Shetani-17

ILIPOISHIA:

“Konso hawa ni ndugu zetu huyu anaitwa Sipe kifupi cha Sipesroza ni mwenyeji wetu lakini anatokea  Gilgil.”

“Gilgil ndiyo wapi?”

“Ipo njia panda ya kutoka Nakuru na Nyahururu kuja  Naivasha kama unakuja Nairobi.”

“Ooh! Nimefurahi kukufahamu.”

“Na huyu anaitwa Bahati ni mwenyeji wa Burundi wote tumekutana hapa tukitafuta maisha na kuwa kama ndugu.”

“Nimefurahi kuwafahamu ndugu zangu.”

SASA ENDELEA…

“Hata sisi,” walijibu kwa pamoja.

“Jamani najua muda ndiyo huu tusiwacheleweshe wahini ili kesho mgeni apate hela ya supu.”

“Asiwe na wasi supu amepata,” alisema Bahati aliyeonekana kuchangamka sana.

“Leo wapi?”

“Koinange.”

“Vipi West Land?”

“Mmh! Jana biashara haikuwa kiviiile tumeona leo tujaribu Koinange maana tuna wiki hatujakanyaga West Land.”

“Mmh! Haya kazi njema.”

Shoga wa Doi aliondoka na kutuacha kujiandaa kupata maji ya kuoga tule  tuzungumze kidogo kisha tupande kitandani. Baada ya kuoga na kujifunga kanga na kujiegeneza mgongo ukutani, Doi aliniambia.

“Konso karibu shoga yangu hapa ndiyo Nairobi mji wa kitalii mji wa kibiashara.”

“Asante.”

“Shoga huu mji tumekuja kutafuta hakuna anayetujua basi tufanye kazi.”

“Sawa Shoga.”

“Nitakuelekeza kila kitu mambo mengine utajua mwenyewe, naweza kusema sisi ni wazoefu kuliko wenzetu tofauti hapa ni Kenya na tulipotoka ni Tanzania. Bei nitakuelekeza kwa vile pesa ya hapa ipo juu kuliko ya kwetu.”

“Sawasawa.”

“Najua hakuna muda wa kupumzika hapa kazi tu au unasemaje?”

“Shoga hatuna ndugu huku, ndugu yetu pesa.”

“Hapo ndipo ninapokukubali Konso, ukisikia pesa hufumbi macho.”

“Moyo wangu na pesa kama samaki na maji.”

“Acha wee, nakuaminia, basi twende tukapate chakula ili tuje tupumzike.”

“Hakuna tatizo.”

Tulikwenda kwenye grosari iliyokuwa jirani na kununua chips mayai na kurudi kulia nyumbani. Huwezi kuamini sikuwa na wazo lolote la kujutia safari yangu ile zaidi ya kujipanga kuwapiku wenzangu kwenye biashara.

 Kwa vile nami nilikuwa na akiba kidogo niliyokujanayo, nilinunua bia mbilimbili tukazimua tukazumgumza sana huku tukitiana ujinga na kujikuta tukilala muda mbaya.

Kutokana na uchovu, niliamka siku ya pili saa nne asubuhi, shoga zetu nao walirudi muda mbaya hivyo kusababisha wote tuchelewe kuamka. Kifungua kinywa siku ile tulipata saa sita kasoro kutokana na kulala muda mrefu.

Siku ile kwa kweli tulishinda tukizungumza mengi na shoga zangu huku wakinieleza  tabia za wanaume wa Nairobi.

 Pia walinieleza pindi nitakapopata mteja wa kulala naye mpaka asubuhi jinsi ya kurudi pale nyumbani kwa urahisi. Kwa kweli maelezo yao yalinifanya nianze kujiamini na kuona naweza kupata mteja wa aina yoyote na kwenda naye bila woga japo nilikuwa sijui mitaa ya Nairobi.

Jioni ya siku ile nami nikaanza kazi yangu rasmi ndani ya Jiji la Nairobi iliyonifanya niandike simulizi hii na kugundua vitu vingi vilivyo nyuma ya mioyo ya watu, tofauti na wasemayo midomoni mwao hata muonekano wa sura zao ulivyo ni tofauti na wawazayo.

Niliweza kuigundua ndoa ya shetani na sisi walimwengu ilivyo ngumu  kuivunja, najua unataka kuijua ndoa hiyo japokuwa wengi tupo ndani ya ndoa na shetani kwa vile kila siku tumekuwa tukiyafanya yale yampendezayo shetani na kumuudhi muumba wetu.

 Nina imani kama bado umo ndani ya ndoa na shetani ni wakati wako kuivunja japokuwa si kazi rahisi.  Basi kama kawaida nami nilijiandaa kuingia mzigoni, vazi nililovaa siku ile lilikuwa tofauti na yao.

Wenzangu walivaa za nusu utupu, mimi nilivaa nguo ya mpira iliyokuwa imenibana  sana na kulionesha umbile langu ambalo kila mwanaume angetamani kuivua nguo  ili aufaidi utamu uliomo ndani yangu. Baada ya kila mtu kuvaa niliposimama mbele ya wenzangu nilimsikia Bahati akisema; “Kama biashara lazima iishe yako ndiyo wengine tuuze.”

“Mmh! Mbona kawaida jamani,” nilisema kwa aibu ya uongo.

“Konso ndugu yangu unatisha kweli umekuja kazini,” alisema Konso huku akinitupia jicho la matamanio.

“Ndo maana yake hatukuja huku kutangaza Injili tupo kikazi zaidi.”

Baada ya kila mtu kuvaa kimtego tuliondoka nyumbani majira ya saa mbili kasoro usiku tukiwa tumejifunga kanga ili majirani wasijue tunafanya kazi gani japo wapo waliokuwa wakijua lakini ilikuwa haiwahusu.

Tulipofika barabarani tulipanda matatuu hadi  Koinange ambako kulikuwa na kijiwe cha wauliza miili. Walikuwepo wanawake na wasichana walioonesha kabisa wengi walikuwa wanafunzi wa vyuo vilivyokuwepo pale Nairobi.

Hilo halikunitisha kwa vile nilikuwa mzoefu wa kazi ile kwa muda mrefu, siku hiyo kijiwe kilikuwa kikavu sana. Baada ya kukaa zaidi ya saa wateja wakionekana wa bei ya chini hata kuja sehemu yetu hawakuweza zaidi ya kwenda kwa wanuka mikojo.

 Nilijiuliza kijiwe mbona kimedorora hivyo, lakini walinipa moyo na kunieleza  muda wa kukata tamaa ulikuwa bado na kibaridi cha Naironi kilikuwa kikichonyota. Majira ya saa nne kasaro wateja wenye magari walianza kutokea kuonesha wengine walikuwa bado wamo maofisini. Kama kawaida yangu sikuwa mtu wa kupigana vibega na watu kukimbilia wanaume, nilijiamini mwanaume mpenda vizuri lazima angenichagua hata kama nikisimama mbali.

Wakiwa watu wakipigana vibega na mimi kusimama, Sipe alipata nafasi ya kupata bwana ambaye aliingia ndani ya gari lake na gari lilikwenda kusimama mbele kidogo ilionekana mteja alitaka huduma ya haraka.

Baada ya dakika ishirini alirudi.

“Vipi?” Doi alimuuliza.

“Ilikuwa huduma ya chapchap si unajua kwa kazi hiyo huwa sicheleweshi.”

“Nakujua.”

Tukiwa katika ya mazungumzo ilisimama gari nyingine, kama kawaida walikimbilia lakini mimi sikunyanyua mguu wangu kitu kilichomuudhi Doi na kuniambia.

“Konso shoga yangu changamka hapa siyo bongo pia kijiwe hujakizoea,” Doi alinishtua.

“Sawa,” nilimjibu huku nikiwa bado nimesimama.

Bahati nzuri kukimbilia kule Doi ilikuwa bahati yake alipata mteja wa kuondoka naye. Nilibakia na shoga zangu wengine ambao ndiyo walikuwa wenyeji wangu. Tulibakia mimi na Bahati ambao tulikuwa hatujapata wateja, majira ya saa nne lilikuja gari moja la kifahari na kusimama karibu na tulipokuwa tumesimama, kama kawaida sikwenda wasichana wote walikimbilia kulizunguka lile gari. Wenzangu walinishika mkono na kunisogeza kwenye gari.

Nilijisogeza hadi karibu na gari ambalo toka lisimsame lilikuwa halijashusha vioo, lilishusha taratibu kisha sauti ilitoka ndani ya gari na kusema:

“Ninyi watatu ingieni ndani ya gari.”

Kila mmoja alijinaji yeye lakini msemaji alimaanisha sisi watatu, tuliingia kwenye gari, lilifungwa mlango na kuondoka bila kusema neno nikajiuliza mbona hakuna maelewano. Niliwaona wenzangu wametulia na mimi nikatulia ili nione mwisho wake.

Je, nini kitaendelea? Usikose Jumamosi ijayo.

Leave a Comment