×

Justine Campos; Msauzi Kimbilio la Mastaa Kibao wa Afrika

Gorilla Films 028 Justine Campos

Mtaani Randburg Gauging jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ndiko zilipo ofisi za Kampuni ya Gorilla Films inayomilikiwa na wapendanao Justine Campos ambaye ni direkta maarufu kwa sasa Afrika na mkewe Candice Campos.

Gorilla Films 010Justine Campos, Davido na wasanii wa Nigeria.

Kutokana na ubora wa video zinazotolewa na kampuni hili pamoja na kuwashika mkono wateja wake, limekuwa kimbilio kwa wasanii wengi wa Kibongo na Afrika kwa ujumla. Katika mahojiano haya ‘exclusive’ kati ya Showbiz na Justine Campos, direkta huyo amefunguka mengi kuhusu kazi zake, wasanii wa Bongo na tasnia ya muziki kwa ujumla, shuka naye;

Gorilla Films 054Msanii wa Marekani, Ace Hood.

Showbiz; Kampuni yako ya Gorilla Films ilianzishwa mwaka gani?
Campos; Mwaka 2002 lakini mwaka 2009 ndipo tulipoungana na Candice na kuanza kufanya kazi pamoja.
Showbiz; Nini mtazamo wako kwa wasanii wa Bongo? Wana uwezo wa kupambana katika soko la kimataifa la muziki?

Gorilla Films 068Campos; Kampuni yangu inajisikia poa sana kufanya kazi na wasanii kutoka Tanzania, ni watu wakarimu kuliko wengine tuliowahi kukutana nao. Kikubwa zaidi ni watu wenye malengo na juhudi, nawapa nafasi kubwa kufanya vizuri kimataifa.

Gorilla Films 122Joh Makin na AKA

Showbiz; Msanii gani unayempenda kuliko wote kutoka Tanzania?
Campos: Ni wengi lakini siwezi kukutajia mmojammoja.
Showbiz: Unafikiri ni nini kinawavutia wasanii wa Kitanzania kufanya kazi na kampuni yako na si kwingineko?

Gorilla Films 140Campos: Bila shaka ni ubora wa kazi zetu, ubunifu, kujali na uzoefu tulionao.
Showbiz: Sasa mnawasaidiaje wasanii mnaofanya nao kazi katika usambazaji wa kazi zao baada ya kuwafanyia prodaksheni kali?
Campos: Hatufanyi kazi ya usambazaji baada ya prodaksheni, labda ambacho huwa tunawasaidia wasanii wengi ni kuwashika mkono kwa kuwatambulisha kwenye vituo vikubwa vya televisheni hasa Afrika.

Gorilla Films 125Vanessa Mdee ‘Vee Money’

Showbiz: Inasemekama mnafanya kazi zenu vizuri sana lakini inadaiwa mnatoza mkwanja mrefu, kwani kwa video mnachukua kiasi gani?
Campos: Kila video ina gharama yake, inategemeana na idea pamoja na mahitaji yatakayohitajika kwa video hiyo.

Gorilla Films 146Showbiz: Kuna vigezo vyovyote vinahitajika ili msanii aweze kupiga mzigo na nyie?
Campos: Hapana, lakini kwa sasa tutahitaji zaidi kufanya kazi na wasanii tuliokwisha fanya nao kazi, wateja wapya hasa wasanii chipukizi hatuwapi nafasi sana labda ikitokea tumependa kazi yake.

Gorilla Films 069Msanii Sarkodie wa Ghana.

Showbiz: Wasanii wangapi wa kimataifa mmeshafanya nao kazi mpaka sasa?
Campos: Ni wengi sana, baadhi wakiwa kwenye video zao wenyewe wengine wakiwa wameshirikishwa. Kwa kuwataja tu baadhi yao ni Ace Hood kutoka Marekani, Sarkodie, Ice Prince, Wizkid, Black Coffee, Vanessa Mdee, Navy Kenzo, Diamond Platnumz, Joh Makini, Hugh Masekela, Nathan Adams, Unathi, AKA, R2Bees, Big Nelo, Oskido, Yannick, Bucie, Yemi Alade, Phyno, Runtown, Uhuru, KO Cashtime, HHP, EL, Davido, Ziyon, The Groove, Yuri Da Cunha, Sauti Sol na Ali Kiba.

Gorilla Films 152Justine Compos na mkewe Candice

Showbiz: Kuna tuzo yoyote mmewahi kupokea?
Kama ndiyo kwenye kipengele kipi na lini?
Campos: Ndiyo, tumepata tuzo nyingi na kuorodheshwa kwenye tuzo mbalimbali. Sina maelezo ya kutosha zaidi kwenye tuzo nyingi ila baadhi ni; Mwaka 2005 nilishindanishwa kwenye kipengele cha Direkta Bora wa Mwaka kwenye Tuzo za SAMA (South African Music Awards).

Showbiz: Unaweza kunitajia wasanii kutoka Afrika Mashariki ambao mmefanya nao kazi?

Gorilla Films 164Jux na video queen.

Campos: Ndiyo, baadhi yao ni Vanessa Mdee, Joh Makini, Navy Kenzo, Jux, G Nako, Ben Pol, Chegg e, Shaa, Kleyah, Diamond Platnumz na Kayumba.
Showbiz: Unaweza kuuzungumzia vipi Muziki wa Bongo Fleva ukipewa nafasi?
Campos: Nafikiri muziki wa Bongo umekuwa wa kisasa zaidi, una maudhui mazuri na kiukweli ninaufurahia tangu nimeanza kuusikia.

Gorilla Films 014Candice akiwa kazini.

Kitu kingine ninawapenda wasanii wa Bongo kwa sababu wana uwezo mzuri wa ‘kuperfomu’ kwenye matamasha pia kwa niaba ya kampuni yangu, nawashukuru Watanzania kwa kufuatilia kazi zetu hata wasanii wake kupenda kufanya kazi na sisi.

Leave a Comment