×

Mama mzazi wa Banza, mtoto wa dada yake wazikwa Dar

5

Majeneza yenye miili ya marehemu yakiwa yanasaliwa.

2

Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Ally Chocky (kushoto) akiwa msibani hapo.

3

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta,  Asha Baraka (katikati) akibadilishana mawazo na wadau msibani hapo.

4

Waombolezaji wakiwa msibani.

6

Waombolezaji wakiwa wamebeba majeneza yenye miili tayari kwenda kuzikwa katika makaburi ya Sinza.

MIILI ya aliyekuwa mama wa msanii wa muziki wa dansi marehemu Ramadhan Masanja ‘Banza’, Khadija Masanja na mjukuu wake Sozi ambao walifariki dunia  jana Jumatatu kwa kupishana saa moja, wamezikwa na kuacha simanzi nzito kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Dua ya mazishi ilifanyika nyumbani kwao Sinza-Lion ambapo watu mbalimbali walihudhuria wakiwemo wasanii wa muziki wa dansi na miili hiyo ilizikwa katika makaburi ya Sinza.

Akizungumza,  kaka wa Banza Stone, Hamis Masanja,  alisema hilo ni pigo kubwa kwao kwani hawakutarajia kwa sababu ni miezi michache tu imepita tangu Banza afariki dunia.

“Ukweli hili ni pigo hata siwezi kuongea mengi, maana inauma sana na hatukutarajia ila ndiyo hivyo imeshatokea hatuna la kufanya, mama ametuacha wapweke sana na tulimzoea jamani sijui tutaishije?” alisema Hamis.

NA GLADNESS MALLYA/GPL

Leave a Comment