ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
“Njoo!” nilimwita moyoni nikasema potelea mbali kama mama Rehema ndiye aliyenitumia meseji…
“Basi nikukute tayaritayari, hakuna kupoteza muda,” aliongeza.
Nilitoka kitandani, nikafungua mlango na kuuacha wazi, nikachojoa nguo, nikarudi kitandani…
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…
Nilikaa mkao wa kusubiri baba Rehema aingie lakini huku akilini nikiwa nina wasiwasi kwamba huenda atakayeingia ni mama Rehema.
Niliuona mlango ukisukumwa polepole, nikainua shingo kuangalia. Baba Rehema akiwa ndani ya bukta tu alizama chumbani kwangu…
“Sogea huko sasa,” aliniambia kwa sauti ya chini, nikasogea…
“Mama Rehema hawezi kushtuka akaja kukutafutia huku kweli?” nilimuuliza…
“Kalala. Akilala amelala yule.”
“Haya sawa.”
Hapo sasa tulikuwa tunazungumza kwa sauti ya chini sana.
Mimi mwili ulishaanza kusisimka, nilikuwa kama naumwa. Kuhema kwangu kulibadilika, nikawa nahema kama niliyetoa kukimbia mbio fupi!
Baba Rehema akaanza kwa kunishika sehemu mbalimbali za mwili. Nikawa najisikia kuzimia kulikokaribia na kupoteza fahamu.
“Jamila,” aliniita…
“Bee…”
“Uko vizuri mtoto… umeumbwa vizuri… hata sijui ni kwa nini uliamua kufanya kazi hii ya ndani mtoto mzuri kama wewe?” aliniuliza huku akiendelea kunishika.
“Hakuna ajira baba Rehema.”
“Mimi nitakutafutia kazi.”
“Kweli baba Rehema?”
“Kweli Jamila.”
Mimi sikujua bwana. Kumbe baba Rehema alikuwa ameshafika mbali na sasa alikuwa anataka kuanza mechi na mimi. Nilikuwa nimeshachoka kila mahali.
“Baba Rehema lakini unanihakikishia usalama wangu kwamba mama Rehema hawezi kuja?”
“Hawezi bwana,” alisema baba Rehema huku sasa tukiwa tumeshaanza mechi.
Kitanda kilikuwa kimelegea, kikaanza kupiga kelele kwachukwachu kwachukwachu…
“Haa! Baba Rehema kitanda kinalia, kitaamsha watu,” nilimwambia baba Rehema. Lakini hakutaka kunisikia, aliendelea kuserereka.
Sasa ikawa kero kubwa kwani mlio wa kitanda ulinifanya mimi nisiwe huru kabisa maana kitanda kilikuwa kikibadili sauti, ikitoka kwachakwachakwacha, inakuja kuchukuchukuchu mara tikitikitiki…
“We baba Rehema…”
“Acha woga wewe,” alinijibu huku akianza kuhema kwa kasi ya ajabu, nikajua mchezo unakwisha. Kweli, baba Rehema akamaliza mchezo lakini sambamba na mimi.
Mlio wa kitanda ukapotea, nikahisi nafuu sasa…
“Baba Rehema nenda,” nilimwambia…
“Kwa nini unanifukuza wakati mi bado?”
“Wee! Acha bwana baba Rehema. Sasa tunakwenda kufumaniwa,” nilijaribu kumtisha…
“Hakuna wa kutufumania bwana, nisikilize mimi.”
Basi, baba Rehema akalala akinikumbatia kama mimi ndiye mke wake sasa.
Kijotojoto nilichokipata kutoka kwenye mikono yake, nikaona faida ya yeye kuwepo kitandani na mimi, nikazidi kujipinda ili iwe kama kuku aliyekumbatia kifaranga chake.
Si tukapitiwa na usingizi bwana, kuja kushtuka hivi, mimi nikaangalia saa, ni saa kumi kasorobo…
“Baba Rehema…baba Rehema…”
“Mh…mh!”
“Saa kumi sasa.”
Baba Rehema alikurupuka, akatoka mbio kwenda chumbani kwake. Nilikwenda kufunga mlango, nikarudi kulala nikisubiri kusikia lolote kutoka huko kwao…
“Da! Sasa je, ingetokea nimeshtuka saa kumi na mbili?” niliuliza mwenyewe huku nikiogopa.
Ilipopita nusu saa, nikajua hakuna kitu, lazima baba Rehema amekuta mkewe hajaamka.
Saa kumi na moja asubuhi niliamka, nikaenda kuanza kazi za ndani kwa kufanya usafi na kuchemsha chai na mambo mengine ya kawaida.
Mama Rehema aliamka akaja jikoni…
“Shikamoo mama.”
“Marhaba, ndiyo unaamka siyo?”
“Hapana mama, nimeamka muda mrefu sana na ndiyo namalizia kazi sasa,” nilimjibu mama Rehema huku nikimwangalia kwa tahadhari kubwa maana alikuwa kama hasomeki sawasawa machoni.
Baada ya hapo mama hakuzungumza tena na mimi mpaka baba Rehema anaamka, akaoga, akanywa chai kisha akaondoka kwenda kazini.
Kwenye saa tano hivi asubuhi, walikuja wageni ambao mimi machoni ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwaona.
Aliwakaribisha, wakakaa sebuleni…
“Jamila,” aliniita mama.
“Abee,” niliitika nikaenda mbio sebuleni. Nikawasalimia wote, kisha nikachuchumaa kumsikiliza mama alichoniitia…
“Jamani, huyu ni hausigeli wangu, anaitwa Jamila. Lakini siku mbili hizi namwona kama anataka kuwa mke mwenzangu. Anajipendekeza sana kwa mume wangu, mimi simpendi kabisa… na iko siku wewe nitakuua tu,” mama Rehema aliporomosha maneno yote hayo huku wale wageni wake wakiniangalia kwa macho makali…
“Mama mimi sina uhusiano wowote na mume wako, wala sina mawazo hayo,” nilianza kujinasua mwenyewe ili kuweka hali salama…
“We koma!” alidakia mmoja wa wale wageni huku akinifuata.
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo.