×

Penzi Kabla ya Kifo-20

Hatimaye bilionea Elizabeth anakutana na mwanaume mwingine, James, maskini ambaye mdogo wake mgonjwa mno. Anapanga kumsaidia binti huyo na kwenda naye nchini India kimatibabu. Huko, hali inakuwa ngumu, moyo wake unaendelea kumpenda James. Unajua nini kilitokea?

SONGA NAYO…

 

Alikuwa kwenye wakati mgumu mno, hakutaka kuona akishindwa hata mara moja, alimhitaji sana James kiasi kwamba wakati mwingine aliona hakuwahi kumhitaji mwanaume moyoni mwake kama alivyomhitaji James.

“James! Ninakupenda kipenzi,” alisema Elizabeth huku maji ya bomba la mvua yakiendelea kummwagikia.

“Kwa nini unanitesa, naomba unikubalie na usinifanyie kama wanaume wengine walioamua kuniumiza, ninahitaji kuwa na wewe tu,” alisema Elizabeth huku akiwa katika hisia kali za kimapenzi.

Alipomaliza kuoga akatoka bafuni kisha kuendelea kujiandaa na baada ya dakika ishirini, walikuwa ndani ya gari maalum lililokuja kuwachukua kwa gharama zake na kuelekea hostelini huku tayari ikiwa imetimia saa kumi na moja jioni.

Katika kipindi chote hicho, Elizabeth alikuwa akijifikiria kama huo ulikuwa muda sahihi wa kumwambia James alivyokuwa akijifikiria au la. Muda ulizidi kuyoyoma, madaktari tayari walikuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakiendelea kumfanyia upasuaji Glory na matokeo kuonesha kwamba uti wake wa mgongo ulikuwa umevunjika kidogo.

“Will she be okey?” (Atapona?) aliuliza Elizabeth.

“We are trying our best, we don’t know yet, but you have to wait,” (Tunajaribu kwa uwezo wetu, bado hatujajua, lakini mnatakiwa kusubiri) alisema Dk. Ajay, alikuwa bingwa wa upasuaji hospitalini hapo.

Walichoambiwa ndicho kilichokuwa kikiendelea. Mbali na Dk. Ajay, pia kulikuwa na madaktari wengi waliokuwa na utaalam wa hali ya juu, kila mmoja mahali hapo alitaka kuhakikisha binti yule mdogo anapona na kuwa kama zamani.

Waliingia kwa zamu ndani ya chumba kile, hakukuwa na kitu walichokuwa wakikisubiri kwa hamu kama kumuona Glory akiwa mzima na hata kama hawatafanikiwa lakini ule upasuaji waliokuwa wakiufanya basi baadaye uweze kusaidia na binti yule mdogo kuwa mzima wa afya.

Baada ya upasuaji kufanyika kwa masaa nane, hapo ndipo madaktari walipowaruhusu kuingia katika chumba cha mapumziko kwa ajili ya kumuona Glory aliyekuwa kimya kitandani. Kila aliyemuona, hakika aliumia moyoni mwake, alikuwa msichana mdogo ambaye hakustahili kupitia mateso kama aliyokuwa akiyapitia mahali hapo.

“Glory! Utapona tu mdogo wangu,” alisema James huku akimwangalia mdogo wake huyo kitandani alipokuwa.

Ilipofika saa nne usiku, wote wakatoka hospitalini hapo na kurudi hotelini. Walipoingia vyumbani mwao, Elizabeth hakutaka kukubali, kiu kubwa ya kufanya mapenzi na James ilimshika kiasi kwamba akashindwa kabisa kuvumilia.

Alichokifanya ni kuoga kisha kuchukua nguo yake ya kulalia tu na kwenda katika korido ambapo akaanza kuugonga mlango wa James aliyefika na kuufungua. Hata kabla hajamuuliza Elizabeth kilichokuwa kikiendelea, akajikuta akisukumwa na kuingia ndani, taulo alilolivaa Elizabeth likatoka mwilini mwake na kumbakiza na nguo ya ndani tu.

“Elizabeth!” alisema James kwa sauti iliyoonesha mshangao mkubwa.

“James! Nakuhitaji, nataka uupoze moyo wangu usiku wa leo!”

“Elizabeth! Are out of your mind?” (Elizabeth! Umechanganyikiwa?)

“No! I want you James! Please, come to me baby!” (Hapana! Ninakuhitaji James! Njoo kwangu mpenzi) alisema Elizabeth.

Hapohapo akamsogelea James na kujikuta wote wakiangukia kitandani. Kasi ya udundaji wa moyo wa James ulikuwa juu mno kiasi kwamba mpaka Elizabeth aliyasikia.

Elizabeth aliumbika mno, kifua chake kilikuwa kizuri, kila James alipokuwa akimwangalia, alijikuta akiingiwa na hamu ya kufanya mapenzi na msichana huyo mrembo. Umbo namba nane, alikuwa na hipsi zilizojengeka vilivyo, nyonga nzuri kiasi kwamba kwa kila mwanaume rijali asingeweza kumuacha msichana kama Elizabeth, tena kwa sehemu kama hiyo, chumbani.

James aliogopa, kwanza hakuamini msichana kama Elizabeth angeweza kukutana naye sehemu kama ile, kila alipomwangalia, wakati mwingine alihisi kama alikuwa ndotoni na kama si hivyo, basi alihisi kulikuwa na jini lililomtokea.

Kulikuwa na wanaume wazuri, wenye fedha ambao kila siku walitamani kulala na msichana huyo, kwake, kila alipokuwa akimwangalia Elizabeth alijiona kuwa na bahati ya ngekewa ambayo hakutakiwa kuichezea kabisa.

Mapigo yake ya moyo yalizidi kuongezeka, kwa mbali, kijasho chembamba kikaanza kumtoka, akajikuta akiwa kwenye wakati mgumu ambao hakuwahi kuwa nao tangu kuzaliwa kwake. Macho yake aliyakaza kumwangalia msichana huyo, alitaka kupata uhakika kama msichana aliyekuwa juu ya kifua chake alikuwa Elizabeth au mtu mwingine.

“Elizabeth….” aliita James kwa sauti ya chini iliyoashiria hofu.

Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

1 Comment

Leave a Comment