×

Kilichosababisha kifo cha Bobbi Kristina hiki hapa

bobbi-kristina-1-768

Bobbi Kristina

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu wa kifo cha aliyekuwa mtoto wa gwiji wa R&B Marekani, Whitney Houston, Bobbi Kristina, hatimaye mamlaka husika imetoa jibu kuwa bangi, pombe na madawa ya kulevya ndiyo chanzo cha mrembo huyo kuondoka duniani.

Bobbi alikutwa akiwa hajitambui bafuni na baadaye kukaa miezi kadhaa akiwa katika hali hiyo ya kutojitambua, kabla ya kukutwa na umauti Julai 26, mwaka jana.
Awali, wanasheria walizuia chanzo cha kifo hicho kutangazwa wakidhani ameuawa na aliyekuwa mpenzi wake, Nick Gordon kabla ya juzikati kutoa ruhusa ya kutangazwa na sasa majibu yaliyotoka ndiyo haya.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Afya cha The Fulton County inadaiwa kuwa marehemu alikuwa ametumia pombe, mchanganyiko wa madawa mbalimbali kama bangi na madawa ya kulevya.
aa
Aidha, ripoti hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi kwa miezi nane, inasema kuwa matumizi yaliyokithiri ya madawa hayo yalisababisha mapafu yake kujaa maji na ubongo wake kudhurika.

Whitney ambaye ni mama wa Bobbi alikuwa amefariki kwenye hoteli moja akiwa ndani ya bafu huku kichwa chake kikiwa ndani ya maji, baada ya kutumia madawa ya kulevya.

Leave a Comment