Kutoka kushoto ni Balozi wa Pakistan hapa Tanzania, Amir Mohammed Khan, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob na Kapteni wa meli ya kivita iliyopa hapa nchini, Ijaz Ahmad.
Kapteni Ijaz (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Meya wa Kinondoni.
Kamanda Ahmad (kulia) akiteta jambo na Meya Jacob kwenye ofisi yake.
Kapteni Ijaz Ahmad (kulia) akimkabidhi sanduku la dawa Meya Jacob.
Wanahabari waliokuwa katika tukio hilo.
Baadhi ya masanduku ya dawa zilizotolewa.
BALOZI wa Pakistan hapa Tanzania, Amir Mohammed Khan na jeshi la wanamaji la Pakistan likiongozwa na Kapteni Ijaz Ahmad ambayo lipo Tanzania kwa siku tatu leo wamemtembelea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob, na kumpa masanduku ya dawa za binadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Khan alisema lengo la kutoa zawadi hizo ni kusaidia hospitali za wilaya ya Kinondoni na kuimarisha mahusiano mema baina ya Pakstan na Tanzania.
Naye Meya wa Kinondoni, Jacob baada ya kupokea msaada huo aliushukuru ubalozi wa Pakistan kwa dawa hizo.
(Na Denis Mtima/Gpl)