×

Pablo Masai: Nipo tayari kuondoka FM Academia

pabloDifumba Kuminga ‘Pablo Masai’.

Imelda  Mtema

MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia, Difumba Kuminga ‘Pablo Masai’ amefunguka kuwa anatamani sana kuihama bendi hiyo lakini sharti lake ni moja tu, masilahi zaidi.

Akizunguimza na mwanahabari wetu hivi karibuni, Pablo aliyedumu  FM Academia kwa zaidi ya miaka 15, alisema mipango yake ni kuendelea kuitumikia bendi hiyo mpaka pale atakapoanzisha yake Mungu akimjalia lakini kama akitokea mtu mwenye kumpa masilahi zaidi, ataondoka FM.

“Natamani kuhama bendi lakini siwezi kuhama bure lazima kuwe na masilahi ya uhakika ya kunifanya nihame hapa nilipo, ama sivyo najipanga nianzishe bendi yangu kwa sababu ninajua uongozi vizuri sana,” alisema Pablo.

Leave a Comment