×

Staric Music Kuachia Bonge la Ngoma Ijumaa

84add12d-c334-4a2a-aed1-a15025b9aaff

KAA tayari wewe unayependa burudani, hit maker wa ngoma ya Kata anakuja na ujio mpya wa ngoma yake aliyoipa jina la Nipe Wakaseme. Wimbo huo anatarajia kuuachia Ijumaa ya wiki hii.

Akipiga stori na mtandao huu, Staric alikuwa na haya ya kunena. “Ujue nimekaa kimya kidogo kusikilizia game linaendaje. Tangu nilipoachia ngoma yangu ya kwanza ya Kata, nimeona namna ambavyo mashabiki wamenisapoti, wamekubari kazi yangu pia.”

53e0412b-0568-4bc9-b477-df8f649c5938Msanii wa Muziki, Staric Richard ‘Staric’.

“Kama ilivyokuwa kwenye wimbo wangu wa kwanza, Nipe Wakaseme ni ngoma nzuri sana, najua itapaa na kikubwa niwaombe mashabiki na wapenzi wa sanaa ya muziki waendelee kuusapoti muziki wangu.”

Kikubwa kabisa wakae mkao wa kula kwani ngoma hii nitaichia soon next week. Nitaachia audio na video vyote kwa pamoja.” alimalizia kusema Staric.

Video mpya ya mkali @staricmusic inaitwa #Nipe_Wakaseme itakuwa on air kwa mara ya kwanza Ijumaa hii. Stay tuned….!

A video posted by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment