×

Malaika: Kuolewa sasa no! Bado niponipo kwanza

12628083_193173931037870_1997683421_nStaa wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’.

Stori: Andrew Carlos
STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza amefungukia ishu yake ya kuolewa ambapo amesema kwa sasa hayupo tayari na kwamba bado yupoyupo kwanza.

Malaika mwenye shepu f’lan ‘amaizing’, aliitonya kona hii kuwa japokuwa anaishi na mchumba wake lakini hilo halimfanyi kufikiria kuolewa akiamini muda wa kuitwa mke rasmi bado.

“Mimi si wa kuolewa sasa bwana! Hapana siwezi kusema nipo tayari, bado niponipo kwanza. Siku ikifika nitawaambia lakini si sasa, nahisi bado muda…si unajua mambo mazuri hayataki haraka?” alisema Malaika

Leave a Comment