Staa mkongwe kunako Bongo Fleva, Prince Dully Sykes akikamua jukwaani.

Sir Juma Nature naye alikuwepo jukwaani kukinukisha.

Staa mkongwe kutoka Wateule, Jaffarai naye alikuwepo kuzikonga nyoyo za mashabiki.
Afande Sele ‘Baba Tunda’ akiwapigia saluti mashabiki mara baada ya kukamua Wimbo wa Mtazamo.

Inspector Haroun ‘Babu’ akikamua Wimbo wa Mtoto wa Geti Kali.

Mmoja wa wasanii wakongwe akikamua jukwaani.

Kundi linalotikisa tangu kitambo la Mabaga Fresh likikamua jukwaani.
Mkali Soggy Dog Hunter naye alikuwepo kumpa tafu Promota Bonga.

Mkali wa nyimbo za Uswahilini, Suma G akikamua jukwaani.

Staa kutoka kundi maarufu la Daz Nundaz, Ferooz akikamua kwa hisia jukwaani.

Ilikuwa burudani! Staa mkongwe, Sister P akifuatilia jambo kwa makini.

Kama karambwanda! Nature haokuona aibu baada ya kukata keki ya Promota Bonga kiisha kujisevia.
Nature akiwa katika picha ya pamoja na Mabaga Fresh pamoja na Sister P.

Mashabiki waliotimba katika shoo hiyo wakishangweka.

Keki iliyoandaliwa kwaajili ya promota Bonga kutimiza miaka 25 kwenye kazi hiyo.

….Akijianda kukata keki.

Akimlisha keki mwanamuziki Juma Nature.

Akimlisha keki Rich One.
AMA kweli! Ng’ombe hazeeki maini, hivyo ndivyo walivyodhihirisha wasanii wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva mara baada ya kuporomosha bonge la shoo katika Mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.
Mkesha huo ulifanyika jana usiku, katika Ufukwe wa Sunrise uliopo Kigamboni jijini Dar uliendana na sherehe ya kutimiza miaka 25 ya promota maarufu nchini, Majid Mdoe ‘Promota Bonga’ . Huku wasaniii kama Afande Sele, Dully Sykes, Jaffarai, Suma G, Manzese Crew, Mabaga Fresh, Zig Zag Crew, Fanani wa Hard Blastaz Crew, Soggy Dog, Inspectour Haruni ‘Babu’ Juma Nature, Sister P, Sold Ground Family Feruzi, Rich One na wengine kibao wakiwakumbusha mashabiki wao kwa muziki uliowahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma.
Shoo hiyo iliandaliwa na na mmoja wa mapromota wakongwe wa muziki huo, Promota Bonga akishirikiana na Kituo cha Redio cha Times FM kilichopo Kawe jijini Dar.
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)