
Naibu waziri wa afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dr .Hamis Kibwangala na Millen Happiness Magese





Naibu waziri wa afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dr .Hamis Kibwangala akielezea jambo kwenye semina


Millen Happiness Magese akielezea jambo




Lady Jay Dee na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifuatilia semina hiyo

MWANAMITINDO wa kimataifa na Miss Tanzania 2001, Millen Happiness Magese kupitia taasisi yake ya Millen Magese inayopambana na ugonjwa hatari kwa jinsia ya kike ujulikanao kama Endometriosis ameamua kuenezea elimu kwa vijana wa kike kuhusu ugonjwa huo hatari duniani kote.
Millen ambaye ni mhanga wa ugonjwa huo katika harakati za kueneza elimu ya ugonjwa huo ameandaa semina kwa vijana wapata 500 wa sekondari pamoja na wazazi, walezi na walimu, semina iliyofanyika kwenye Sekondari ya Turiani, Magomeni hasa kuwapa elimu watoto wa kike kuachana na dhana potofu ya kutojitokeza kama Millen alivyojitokeza.
Akizungumza katika semina hiyo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangala, Millen alijikuta akimwaga machozi stejini wakati akieleza ugonjwa huo ulivyotibua ndoto zake za kupata mtoto huku pia akiwa amefanyiwa upasuaji mara 13.
“Siyo kusema niko hapa kujitangaza kwa manufaa yangu, ni kwa nyinyi wadogo zangu, mimi zamu yangu imeishaisha, ugonjwa huu ni hatari sana, jitokezeni kusema uwazi msaidiwe. Nimekaa na ugonjwa huu miaka 23, nimefanyiwa upasuaji mara 13, ndoto yangu ilikuwa nami siku moja niitwe mama, lakini ni Endo imeharibu ndoto yangu. Naomba serikali iweke jitihada zote kutafuta chanzo cha tatizo hili haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya wadogo zangu.
“Kupitia taasisi yangu nimepanga kueneza elimu ya ugonjwa huu mkoa kwa mkoa, kijiji kwa kijiji ili kila mmoja atambue hatari ya ugonjwa huu,” alisema huku machozi yakitiririka huku baadhi ya wanawake wengine wakianza kulia ukumbini hapo.
Daktari kutoka Chuo cha Muhimbili, Faudhul Alwy aliyeendesha semina hiyo alisema inakadiriwa wanawake milioni 176 wana ugonjwa huo huku 50% ya wanaopata maumivu wakati wa hedhi wana tatizo hilo. Dalili za ugonjwa huo ni maumivu wakati wa hedhi ambayo huweza kuenea mpaka kwenye nyongo, tatizo la kutopata mtoto na wakati mwingine kukohoa damu.
Aidha changamoto kubwa mpaka sasa ugonjwa huo haina dawa huku ukitajwa kuwa na gharama kubwa zaidi ambapo kila mwezi humhitaji mgonjwa kutumia zaidi ya milioni mbili katika kutuliza maivumivu ikiwemo kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo serikali kupitia naibu Kigwangala alisema wamepanga kuboresha mfumo na huduma za afya kwa wanawake ikiwemo kuanzisha mfuko kwa kila mtu na kila mmoja atakuwa na bima kwa ajili ya matibabu.
Semina hiyo ilihudhuriwa pia na mastaa kama Lady Jay Dee, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Lilian Kamanzima, Genevieve Mpangala Nasreem Khareem na Tausi.