
Msomaji wa magazeti ya Global Publishers Ltds, akichanganya kuponi ili kuwapata washindi wa droo ya tatu ya Shinda Nyumba jana.

Msomaji huyo akisoma jina na mmojawapo wa washindi wa droo ya tatu ya Shinda Nyumba.


Wasomaji hawa wakichangamkia fursa wakati wa droo hiyo.

Burudani zikiwa zimepamba moto wakati wa droo ya tatu ya Shindano la Shinda Nyumba.

Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) akimpongeza Godfrey Mpiluka aliyejishindia zawadi za papo kwa papo mara tatu.

Orodha ya washindi wa droo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
DROO ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na kampuni inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Amani, Championi, Ijumaa, Risasi na Ijumaa wikienda, Global Publishers ilifanyika jana, Machi 30 katika Viwanja vya Manzese-Bakhresa jijini Dar es Salaam.
Katika droo hiyo iliyohudhuriwa na umati, Zalika Ally wa Lushoto aliibuka mshindi wa TV Flat Screen na king’amuzi cha Ting huku Charles Elia Chawala wa Dar akijipatia zawadi ya simu ya kisasa ya Smart Phone.
(Picha na Richard Bukos / GPL)