×

Ben pol afungukia kukwama kolabo na Tiwa

zbenpol

Benard Paul ‘Ben Pol’

Na Boniphace Ngumije

MKALI wa Muziki wa R&B Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ amefunguka kuwa kutokana na ziara za kikazi alizonazo mwanamuziki anayekimbiza kwa sasa Afrika Magharibi, Kati na Mashariki, Tiwa Savage kutoka Nigeria zimechangia kushindikana kufanyika kwa kazi yao mpya waliyokuwa wamepanga kufanya hivi karibuni.Tiwa-Savage1

Tiwa Savage

Akichonga na Showbiz, Ben Pol alisema imewabidi kuisogeza mbele projekti yao hiyo anayofikiri baada ya Tiwa Savage kumaliza ziara zake za kikazi anazofanya kwenye nchi za Asia watakuwa na nafasi ya kutosha kukutana na kufanya kazi nzuri.

“Tiwa sasa yuko bize, namsubiri amalize ziara zake na mambo yakienda sawa tutakuja na ujio ambao mashabiki wangu na wake wataufurahia muziki mzuri kwa sababu nimejipanga vilivyo kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa,” alisema Ben Pol.

Leave a Comment