
Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo’
Andrew Carlos
Staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo’, anatarajiwa kushuka Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kupiga shoo ya ‘live’ kwa kutumia vyombo.
Akizungumza na Showbiz Extra, mmoja wa waratibu wa shoo hiyo iliyopewa jina la Jembeka Festival 2016, Michael ‘DJ Kflip’ alisema kuwa Ne-Yo atatua na timu nzima ya watu 22 wakiwemo madansa ambapo watakamua shoo ya kutumia vyombo mwanzo mwisho.
“Itakuwa shoo ya kihistoria kwa Jiji la Mwanza kwani Ne-Yo amejipanga vya kutosha akiwa sambamba na madansa wake,” alisema DJ Kflip.
Katika shoo hiyo, staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond naye atakuwepo kumsindikiza Ne-Yo huku mastaa kibao wa Bongo Fleva kutoka Dar na Mwanza wakilitawala jukwaa.
Shoo hiyo imedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.