Mambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii ya Mapishi ya Leo? Naamini uko vizuri na unaendelea na majukumu yako kama kawaida, kama kawaida ya kila Jumamosi, leo tunajifunza kupika mlenda wa majani ya maboga kama wengi walivyoomba.
MAHITAJI
Bamia
Majani ya maboga
Nyanya chungu (kama utapenda)
Magadi
Chumvi
Karanga zilizosagwa
Maji
KUTAYARISHA NA KUPIKA
Osha na kata bamia na nyanya chungu vipande vidogovidogo
Chambua majani ya maboga na yaoshe vizuri kisha kata ndogondogo
Bandika maji mpaka yachemke
Weka chumvi na magadi
Weka majani ya maboga, bamia na nyanya chungu
Acha vichemke kwa dakika 5.
Weka unga wa karanga na acha uchemke kwa dakika 10.
Hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kula, nzuri kuliwa na ugali