Na Andrew Carlos
MASTAA kibao wa Muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na Stamina, Mo Music, Barakah Da Prince pamoja na Juma Nature wanatarajiwa kumsindikiza mkali wa Muziki wa R&B kutoka Marekani atakayetua jijini Mwanza kwa mara ya kwanza Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba.
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa waratibu wa shoo hiyo iliyopewa jina la Jembe Festival 2016, Kevin Michael ‘DJ Kflip’ alisema kuwa hadi sasa listi ya mastaa wa Muziki wa Bongo Fleva watakaomsindikiza jamaa huyo inaongezeka.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Jiji la Mwanza, Ne-Yo atashuka na kufanya shoo ambayo haijawahi kutokea huku akikaribishwa na staa wa Bongo Fleva anayetikisa, Diamond Platnumz,” alisema DJ Kflip.
Wasanii wengine watakasindikiza ni pamoja na Ruby, Maua Sama.
Shoo hiyo imedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers.