
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji anayetokea hapahapa Tanzania ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta amezidi kufanya vizuri na kuuthibitishia ulimwengu wa soka na mashabiki wake kuwa kiwango chake kwenye tasnia hiyo kimezidi kukua na kumletea mafanikio kila kuchwao.
Jana usiku Samatta amerithibitisha hilo baada ya kupachika bao la tatu dakika ya 77 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis kwenye mechi yao dhidi ya KV Oostende.
Samatta alifunga bao hilo baada ya kutumia vyema pasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Neeskens Kebano. Goli hilo linakuwa goli la tatu kwa Samatta toka ajiunge na klabu ya KRC Genk. Mpaka dakika ya mwisho KRC Genk 4-0 KV Oostende.
TAZAMA VIDEO YA GOLI LA SAMATTA