
Baadhi ya washiriki wa Shika Ndinga wakishikilia chupa za maji katika hatua ya kwanza.

Washiriki upande wa akina mama wakijiandaa kwa mzunguko wa kwanza.

…Wakishikilia chupa za maji ambapo anayeshindwa kuvumilia katika hatua hiyo anakuwa amejiondoa kwenye mchuano.

Baadhi yao wakiwa katika mapumziko.

Washiriki wakiwa katika mzunguko wa nne.

Baadhi ya mashabiki wakifuatilia shindano hilo la Shika Ndinga.

Watu wa huduma ya kwanza wakitoa huduma kwa baadhi ya washiriki walioshindwa kuvumilia.

Washiriki wakiwa katika hatua ya mwisho ya kushika glasi za maji huku wakishikilia gari kuwapata washindi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Efm wakifuatilia shindano hilo.

Mwanamama aliyeibuka kuwa mshindi wa pikipiki baada ya kushika ndinga kutoka Wilaya ya Temeke, Philipina Msanga.

Mshindi wa upande wa akina baba aliyeibuka kidedea kwenye shindano hilo.
SHINDANO la Shika Ndinga linaloratibiwa na Kituo cha Redio cha Efm kilichopo Kawe jijini Dar er Salaam, jana lilizinduliwa rasmi katika Viwanja vya Zakhem, Temeke jijini Dar.
Shindano hilo limekuja ikiwa ni mara nyingine baada ya kufanyika mwaka jana na kupatikana washindi, ambapo kwa mwaka huu limezikutanisha wilaya za Ilala; Kinondoni, Temeke na wilaya mbili za Mkoa wa Pwani ambazo ni Bagamoyo na Kibaha.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Efm redio, Dennis Ssebo alisema kuwa shindano hilo limenza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao ambao ni wanawake watano na wanume watano wataingia katika fainali kujinyakulia gari aina ya Suzuki Carry.
Aidha Ssebo alisema kuwa mwaka huu shindano hilo limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali hivyo akaongeza kuwa washiriki hao walipatikana kutokana na kujibu maswali kwa ufasaha kupitia vipindi vya Efm redio.
Kwa upande mwingine alisema lengo la shindano hilo ni kuwawezesha wasikilizaji wa Efm kwa namna moja au nyingine kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
(Picha/Stori: Hilaly Daud na Denis Mtima/GPL)