×

Aaiii… Wewee…!-5

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Msoba yeye baada ya kukaa tu na kumwona Sada amekaa jirani pale, alisimama kuwafuata huku akitembea kwa mwendo wenye kisasi ndani yake.
Sanura alishangaa, akabaki ametoa macho kumwangalia atafanya nini…

JIACHIE MWENYEWE SASA…


Kumbe huyu mwanaume ndiye aliyekuwa anakupa ujinga na kunifanyia vitimbi vingi ili nikuache siyo?” alisema kwa kufoka Msoba huku akimwelekea Jalia.

Jalia alisimama akitaka kupambana…
“Unasemaje wewe? Mbona wewe uko na mtalaka wangu yule Sanura, mimi nimesema nini?” alijitetea Jalia…
Msoba alishtuka kusikia kwamba, yule ni mume wa Sanura akasita kuendelea…
“Ina maana…hebu Sanura njoo,” Msoba alimwitia Sanura pale kwenye meza ya akina Jalia.
Sanura alikwenda akitetemeka kwani alikuwa anajua ubabe wa Jalia…
“Eti huyu ndiye mtalaka wako?” aliuliza Msoba…
“Ndiyo…”
“Kha! Inakuaje mtalaka wako wewe awe na mtalaka wangu mimi halafu mimi niwe na wewe! Kuna nini katikati yetu?” alihoji Msoba huku akikaa. Alionesha kuchoka kabisa…
“Hata mimi mwenyewe nashangaa sana,” alisema Jalia…
“Hata mimi,” alidakia Sada.

Waliamua kukaa pamoja hapo ili kuzika tofauti zao za nyuma ili kila mmoja aendelee na aliyenaye kwa sasa.
Msoba ndiye aliyekuwa mzungumzaji mkubwa akisema kama wamebaini hivyo basi wawe marafiki kwani kila upande mmoja unapajua nyumbani kwa upande mwingine…
“Maana najua Sanura anapajua nyumbani kwako bwana Jalia kama vile Sada anavyopajua nyumbani kwangu,” alisema Msoba.
Mwisho wa yote walishikana mikono na kuendelea na kuendelea na vinywaji huku amani ikitawala tofauti na awali kwani wote katika kuachana kwao walitawaliwa na uadui mkubwa.

Sada alitumia nafasi hiyohiyo ya amani kumtumia meseji Msoba…
“Lakini mh! Nimekukumbuka mume wangu wa zamani? Nimekuona nimekumbuka mavituz yako…”
“Mimi je? Ndiyo maana nilitaka kupigana hapa…”
“Teh! Teh! Sasa itakuaje jamani?”
“Wewe unatakaje?”
“Japo leo basi tukutane mahali tukumbushane.”
“Wapi, saa ngapi?”
“Nitakusikiliza wewe tu.”
Wakati Msoba na Sada wakichati hivyo, Jalia naye alianza kwa Sanura…
“Kumbe huyu jamaa ndiye anayekuweka mjini sasa!”
“Ha! Ha! Na wewe si unamuweka huyo..!”
“Da! Nasikia wivu…”
“Umeanza mambo yako Jalia…wivu wa nini wakati uliniacha mwenyewe tena kwa talaka tatu…”
“Hasira zile mke wangu…”
“Si umeona sasa, hasira hasara…mwenzio kajitwalia kama wewe naye ulivyomtwaa wa kwake…teh! Teh!”
“Da! Yaani nimekumisi kweli Sanura wangu…”
“Mimi pia my dear…”
“Sasa?”
“Wewe unasemaje?”
“Nataka leo tukakumbushie…”
“Saa ngapi?”
“Wewe nafasi yako…”
“Mimi nafasi yangu hata nikitoka hapa tunaweza.”
“Basi tukitoka, wewe nenda kanisubiri pale tulipokuwa tunakulaga baga wikiendi.”
“Sawa, nitakwenda. Da! Miss you sana Jalia wangu…”
“Mimi zaidi Sanura.”
Wakati Jalia na Sanura wakifikia hatua hiyo, Sada na Msoba walishakubaliana nao wakutane pale walipokuwa wanakwenda kula mishikaki…
“Poa, nani ataanza kufika sasa?” Sada alimuuliza Msoba…
“Yeyote yule…”
“Poapoa mume wangu wa zamani…”
“Jamani mnajua hapa tuko watu zaidi ya kumi,” alisema Jalia huku akicheka kisha akafafanua…
“Maana kama mimi nachati na watu wawili mfano, Sanura pia, Sada hapa vilevile na bwana mzee pia. Mnadhani tuko wangapi? Maana wote tupo kimya na tumeinamia kwenye simu zetu.”
Wengine walicheka sana halafu wakasema kwa pamoja…
“Tena kweli bwana.”
“Sasa nadhani sisi tuondoke,” alisema Msoba akijiandaa kusimama baada ya kulipa vinywaji vyote…
“Sawa, tunashukuru sana jamani. Itabidi siku moja tutembeleane,” alisema Jalia akimwangalia Sanura.
Msoba na Sanura waliondoka, mbele Sanura akamwambia Msoba…
“Baby inabidi niende Kimara kwa mama mdogo, wewe si unakwenda nyumbani kwako?”
“Hapana! Japokuwa awali tulipanga twende wote nyumbani lakini na mimi nina safari ya ghafla pale  nilikuwa nachati na sista wa Magomeni, inabidi niende.”

* * *
Sada alivunja ukimya wakiwa bado wamekaa pale mgahawani…
“Sweet, unajua hapa nilikuwa nachati na anti Salma, kasema niende kwake…sasa itakuaje na tulipanga twende Coco Beach..?”

JE,NINI KILIENDELEA?
USIKOSE KUSOMA WIKI IJAYO

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave a Comment