Mrembo akishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta anamwaga machozi
KWELI mtume hakubaliki nyumbani! Hayo ndiyo yaliyotokea kwa mashabiki wa kike wa Mali ambako wanamuziki Flavour, Mr 2Kay na J Martins walifanya shoo ambayo kutokana na ‘mizinguo’, iliwatoa machozi mashabiki wa kike ambao walilia bila kujua kilichokuwa kikiwatokea kutokana na utamu wa muziki walioupiga.
Watu walisema vilio vya mademu hao wa Mali ni kitu ambacho ni adimu kwa wasichana wa Nigeria kutokea, jambo linalothibitisha kwamba mtume huwa hakubaliki nyumbani.