×

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo 17

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
“Jamila, mbona lipo wazi hilo?” mama Rehema alinipaka matope yake bila kujali athari ya mazungumzo hayo…
“Wewe umejisahau siyo unavyotembea na vitoto vidogovidogo na wewe limama lijitu lizima?” baba Rehema alimtupia kijembe…
SHUKA NAYO MWENYEWE…

Yeye Jamila! Je, anavyotembea na yule baba mwenye virusi uliyeniambia siku zile tunatoka msibani kwamba anatumia dawa za kuongeza siku za kuishi hujamwona umeniona mimi tu siyo?”
Ghafla nilimwona baba Rehema akikata simu na kunigeukia mimi huku akiwa amenitumbulia macho…
“Jamila…”
“Abee…”
“Unaweza kunidanganya mimi..?”
“Kuhusu nini mpenzi wangu?” nilijifanya kumuuliza kama vile sijasikia alichouliza wakati nilijua kila kitu…
“Kumbe unatembea na mwathirika?”
“Mimi Jamila?” nilimuuliza ili kumuweka katika mazingira ambayo yangemfanya na yeye ajue nasingiziwa…
“Wewe Jamila ndiyo kwani naongea na nani hapa?”
“Unaongea na mimi Jamila…”
“Unatembea na yule mzee mwenye virusi?”
“Mama muongo. Nichukue ukanipime sasa hivi…nipime mimi tu, usijipime wewe…kama nina virusi ninyongelee mbali…asitake kunigombanisha kwa makusudi…
“Nilishakwambia kwamba sijawahi kuwa na mwanaume hapa mtaani. Si vijana si wazee achilia mbali wenye virusi. Mimi kwanza ni muoga sana, ujasiri umenipa wewe ndiyo maana nilikuwa nakataa hata kukukubalia maana nilijua cha mtu…
“Hao vijana wa mtaani nawajua, wao ni wenyeji mimi ni mgeni. Sasa unataka kuniambia hawana wapenzi wao? Si wanao! Mimi sipendi kuingilia mapenzi ya mtu mwingine kwani najua inaweza kuzuka fujo…
“Huyo mzee mwenye virusi sina hata haja ya kukuuliza ni yupi maana sijawahi kuwa na uhusiano na mtu mzee, si hapa wala si nilikotoka,” nilisemna sana mpaka nikamwona baba Rehema akiachia tabasamu…
“Jamila,” aliita…
“Jina langu…”
“Du! Yule mama Rehema anakuonea wivu nimegundua hilo…”
“Usiseme hivyo mpenzi wangu labda ana ushahidi mkubwa mikononi mwake ila kama hana basi ana lake jambo kuhusu mimi na sitakubali kwa kweli.”
“Hana lolote yule, mzinguaji tu. Na tena nataka kukuhakikishia kwamba ili kumuweza, nabadili namba ya simu asinipate hewani maana akinipata atakuwa ananisumbua sana.”
“Hapo hata mimi nakuunga mkono wa kulia mume wangu. Ndiyo maana nikasema mimi nikishika nafasi ya umama wa nyumba hii, ndipo mama Rehema atakapojua kumbe kuna vichaa kama yeye hapa duniani…”
“Umama wa nyumba hii umepata kuanzia leo tena muda huu.”
Nilifurahi sana, nikamkumbatia na kumbusu. Kwa vile nilishajua udhaifu wa baba Rehema, nilisimama, nikamshika mkono na kumwambia…
“Twende chumbani mpenzi wangu.”
Alisimama haraka sana. Baba Rehema alipenda sana ‘mambo yale’ hivyo alisimama kama amepigwa na shoti ya umeme alipokaa…
“Twende baby,” alisema tukianza kutembea kwenda ndani.
Kufika chumbani, nilimsaidia kuchojoa nguo ili awe huru na nilimwambia nataka awe huru…
“Kweli hata mimi leo nahisi kwamba natakiwa kuwa huru,” alisema.
Nilimpandisha kitandani, nikamlaza huku nikimfunika na kanga yangu moja. Hivyo hapo mimi nikawa sina nguo.
Nilipenda kucheza naye baba Rehema kwa muda huo. Si tayari nimepewa umama wa nyumba kubwa kama ile!
Tulicheza, tukacheza mpaka tukachezeana. Baba Rehema akafika eneo lake akapata.
***
Mlio wa geti kugongwa, Rehema akiwa amerudi kutoka shuleni ndiyo uliotufanya tuamke. Mimi nilikwenda kumfungulia lakini kwa tahadhari maana awali tulijua ni mama Rehema na timu yake na baba Rehema nilimwambia asitoke kitandani maana nilijua kama saa zile alitoka na bastola, safari hii angeweza kutoka na bunduki kabisa.
Muda ule niliposema wakati natoka chumbani nilisikia paa! Ilikuwa paa ya mlango mkubwa na si ya mlio wa bastola aliyotoka nayo baba Rehema. Ila wakati tunakwenda chumbani kujipumzisha bastola aliiacha sebuleni kwenye kochi akisema hakuna atakayeingia.
Na kweli, kwa jinsi nyumba ilivyo, hawezi mtu kuingia sebuleni au ndani bila idhini ya mtu aliye ndani.
Kwa hiyo nilimfungulia geti Rehema, anaingia tu, akauliza…
“Mama yuko wapi?”
“Alipoondoka muda ule alirudi akafanya fujo zake hapa akaondoka. Hatujajua amekwenda wapi?”
“Ha! Ina maana mama amekuachia nyumba wewe dada Jamila?”
“Mimi ndiyo mama yako kuanzia sasa hivi…”
“Mimi sitaki wewe uwe mama yangu…baba yangu hawezi kuoa mwanamke kama wewe, jiangalie kwanza…” mtoto Rehema alinifyatukia licha ya umri wake kuwa mdogo mpaka nikashangaa mwenyewe…
“Rehema nakwenda kukusemea kwa mume wangu ambaye ni baba yako,” nilimwambia nikiwa naingia chumbani kwa baba yake.
Nilisukuma mlango wa chumbani kwa kasi kama kuna ugomvi nikiwa nimemwacha Rehema sebuleni…
“Mume wangu kwa nini mtoto wako ananitukana?” nilisema nikianza kulia kwa baba Rehema…
“Sijakauelewa mke wangu!”
“Rehema amenitukana sana, hivi hapa afadhali niondoke kwenye nyumba hii,” nilisema nikichukua kanga na kuivaa…
“Yuko wapi?”
“Sebuleni…”
Baba Rehema alitoka kitandani, akaninyang’anya kanga, akajifunga na kutoka. Mimi nilitoka na taulo lake ili nikasikilize…
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

1 Comment

Leave a Comment