Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa kutoka msimu huu tulionao sasa.
Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.
Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.
SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa mafua.
Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.
VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Kitunguu saumu kinatoa kinga hali kadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua.
Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.
MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba, ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua.
Machungwa ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C. Pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Itaendelea wiki ijayo.