Korede Bello akiwa na Wizkid.
MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria anayerekodi kupitia kampuni ya Mavin Records, Korede Bello, na ambaye hivi karibuni ametoa video yake ya ‘Mungo Park’ ambayo inatamba vilivyo katika anga za muziki, anasemekana huenda akafanya kolabo na mwanamuziki mwingine nyota wa Nigeria, Wizkid.
Wapenzi wa muziki wanaona hilo linawezekana hususani baada ya Korede, mwanamuziki ambaye anaonyesha juhudi kubwa kukidhi kiu ya mashabiki wake, kutoa picha katika ukurasa wa mtandao wake akiwa na Wizkid.
