×

Madai ya Wizi wa Marehemu Ajalini, Tunda Man Abanwa

Tundaman (2)Staa wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ pamoja na marehemu Man Katuzo.

NYUMA ya ajali ya gari ndogo aina ya Toyota Aurion iliyotajwa kumhusisha staa wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ kumeibuka maswali matano yanayombana msanii huyo kutokana na mazingira ya tukio zima.

  • ENEO LA AJALI
  • Ajali hiyo ilitokea Jumapili iliyopita maeneo ya Makambako wakati staa huyo akitokea mkoani Njombe kufanya shoo ambapo taarifa zilieleza kuwa, dereva wa gari hiyo iliyosemekana alikuwemo Tunda Man na wenzake wawili, Man Katuzo alifariki dunia papohapo.

Tundaman (5)Ajali ilivyotokea

  • MASWALI YENYEWE ALIYOBANWA TUNDA HAYA HAPA!
  • Swali la kwanza; inakuwaje gari ipate ajali, iwe nyang’anyang’a kiasi kile halafu Tunda atoke bila majeraha wakati wenzake wawili walionusurika wote wana hali mbaya?
  • Swali la pili; kwa nini Tunda Man alisema marehemu alikuwa ni dereva wake kitu ambacho kilimfanya kaka wa marehemu aibuke na kukanusha kuwa marehemu alikuwa ni bosi wao na ndiye aliyewagharamia kwa kila kitu kutoka Dar hadi Njombe walipokwenda kufanya shoo?

Tundaman (4)

Swali la tatu; kama ni kweli walipata ajali pamoja na marehemu, alipataje ujasiri wa kuchukua vifaa vya marehemu vyenye thamani kubwa; kamera 2 aina ya 5d na Mac3  kuviweka kwenye gari nyingine (Toyota Noah) kisha kuondoka navyo hadi polisi walipowazuia na kukutwa na vifaa hivyo?

Swali la nne; kwa nini kaka wa marehemu alilalamika kuwa alimpigia simu Tunda kuhusu taratibu za mazishi lakini hakupokea?

Swali la tano; kwa nini Tunda ameshindwa kuhudhuria mazishi ya mtu waliyekuwa naye msafara mmoja halafu aishie kutoa pole kwenye mitandao ya kijamii wakati marehemu alikuwa mtu wake wa karibu kiasi cha kushirikiana katika wimbo?

  • Baada ya Gazeti la Ijumma kumbana Tunda Man amefunguka kila kitu.

KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA IJUMAA, LEO April 22, 2016

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment