×

Mkumbuke… Noorah Mwana Chemba aliyefichwa na ajali!

noorah

 Haji Nurah Noorah au Baba Stylz

Na Gabriel Ng’osha
“…oyeee niko na Sumalee with Roy ndani ya G Records Chemba Squad, ebwana Ibraa yeee utaipenda hii… akatizapo kila street midume nyoyo zapwita, akikukata kijicho tu ni kama anakwita uuuh anawachengua matoziii mtoto anayejua

mapooziii…,” hiyo ilikuwa ni ‘intro’ ya wimbo wa Ice Cream wa mkongwe wa Bongo Fleva, Haji Nurah Ngarama ‘Noorah’.
Noorah au Baba Stylz kama wengine wanavyomfahamu, aliufanya wimbo huo mwaka 2007 ndani ya Studio za G-Records, Bongo Dar es Salaam. Ana heshima kubwa kwenye muziki, staili yake nzuri ya kucheza na maneno ndiyo ilimfanya apendwe zaidi.

noorah (1)

Safari yake ya muziki ilianzia kwenye Kundi la Chemba Squad lililokuwa na vichwa vikali kama Albert Mangwea ‘Ngwea’, (marehemu), Athuman Kabongo ‘Dark Master’ na Moses Bushagama ‘Mez B’ ambalo chimbuko lake lilikuwa ni Dodoma. Kwenye makala haya Noorah amefunguka mengi:

Awakumbusha mashabiki alikotokea, “Mwaka 2000 ndipo rasmi nilipoanza kuingia kwenye muziki baada ya Sebastian Maganga kuvutiwa na kipaji changu na kuniwezesha kufanya wimbo wa Vijimambo na Wameiba Pombe.

 MezB1

Mez B

Amtaja aliyetoa wazo la nyimbo hizo
“Nyimbo zote zilikuwa ni mawazo ya Seba (Sebastian) na ziliandikwa na Eluka. Baada ya hapo nikatoa Hanitaki chini ya usimamizi wa Abdiel Mengi pale Backyard Records. Ikafuata Ice Cream ambayo niliifanya chini ya Venture Kilosa na tukafanikiwa kutoa albamu ya The Baba Stylz mwaka 2006.

Mapokezi ya The Baba Stylz
“Haikufanya vizuri sana kwa sababu matangazo hayakuwa ya kutosha na nyimbo nyingi watu hawakuzielewa. Nikaendelea na harakati kisha baadaye niliamua kwenda Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) hadi mwaka 2010 ambapo nilipumzika muziki.

5Marehemu Ngwea

Kilichofuata…
“Nilitoa wimbo wa Chambervernment ft Ngwea na Lugha Gongana ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa B’Hitz, nikatoa Nikupe Nini ft Ali Kiba na Acha Ushamba ft Dully Sykes na Chegge. Mwaka 2013 nilifunga ndoa na mke wangu mpendwa Anna Kigwalu ambapo mwaka huohuo ndiyo tulimpoteza Ngwea.

Ukimya kwenye gemu
“Ni suala la mpangilio wa maisha kwa sasa niko nyumbani Shinyanga napumzika kidogo. Tuna kazi mpya ambayo tumefanya ila kikubwa ninachofanya ni kupumzika kufuata ushauri wa daktari.

Afafanua tatizo
“Ni kutokana na ajali mbaya niliyoipata mwaka 2005 nikiwa kwenye Tour ya Fiesta, katika ajali ile sehemu ya fuvu la kichwa changu liligundulika kupata ufa, nilienda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi ndipo daktari aliponishauri kuwa natakiwa nipumzike kwa muda.

Kuhusu kupotea kwa Chemba Squad
“Si rahisi kwa Chamber Squad kupotea, tulibaki mimi na Dark Master ila baadaye tukamuongeza mdogo wake Mez B anaitwa One Six na tayari tumeshafanya ngoma moja inayoitwa Yes Boss. Tunatafuta ‘management’ ya kuisimamia ndiyo tuiweke mtaani.

Mikakati yao kwa sasa
“Bado tuko na tunajipanga kufanya mambo makubwa sana kwa siku zijazo. Sisi tunacheza karata zetu kwani hatuwezi kuwa kama Diamond au Joh Makini. Noorah nitabaki kuwa Noorah na nina mashabiki wangu wananisapoti na vivyo hivyo kwa Dark na One Six.

Anachokikumbuka kutoka kwa memba wa Chemba
“Walikuwa wacheshi na wenye upendo wa dhati, kwa mfano Ngwea alikuwa ni ‘mult talented’. Aliweza kuimba na kurap. Ni msanii aliyekuwa na uwezo wa kufanya free style za kipekee, naweza kusema hajatokea msanii kama yeye.

Kumbukumbu ya majonzi
“Mwaka 2014 mimi na mke wangu tulipopata matatizo ya kiafya ambayo yalidumu kwa muda  mrefu hadi Machi, 2015 mke wangu alipotangulia mbele ya haki wakati huo nilikuwa na wiki moja nyuma nimetoka kumzika rafiki yangu Mez B.

Tujikumbushe
Chemba Squad ilianzishwa 1999 wakati Ngwea, Mez B, Dark Master, Noorah na wengine wakiwa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Mazengo mjini Dodoma na baadaye walikita maskani yao jijini Dar na kufanya kazi kibao kwenye gemu la muziki wa Kibongo.

 

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment