Picha iliyokuwa ikipita katika TV iliyokuwa ukutani kuashiria uzinduzi huo.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki Miss Dar City Centre wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi wa uzinduzi wa mashindano hayo, Zainul Dossa, akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa mashindano hayo ya Miss Dar City Centre.
Mwakilishi wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda, ambao ni wadhamini wa mashindano kupitia Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba akiongea machache kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakipata ‘selfie’ katika ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa.


…Wakiendelea kupiga picha kwenye ‘red carpet’.
Mmoja wa washiriki wa mashindano hayo akipozi katika ‘red carpet’.

Warembo wakiendelea kupozi mbele ya kamera.
Washiriki wa Miss Redd’s mwaka 2014, Sabrina Thomas (kushoto) na Catherine Kisaka, wakiwa katika pozi.

Mratibu wa mashindano hayo, Nancy Josephy (katikati) akipozi na wageni waalikwa.

Warembo wakipozi sehemu yao.
SHINDANO la kusaka warembo lijulikanalo kama Zan Aqua Miss Dar City Centre limezinduliwa rasmi jana, Aprili 23 ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip City Centre jijini Dar.
Mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph alisema shindano hilo litafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip City Centre huku akiahidi kwamba watayarishaji wamejipanga kulifanya liwe la kipekee kuliko mashindano yaliyotangulia.
Mara ya mwisho kufanyika shindano hili lilikuwa likitambulika kama Redd’s Miss Dar City Centre ambapo ilikuwa mwaka 2014 na mrembo Jihan Dimechk aliibuka kidedea.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mgeni rasmi wa mashindano hayo, Zainul Dossa, alisema kuwa mashindano hayo ni moja ya ajira katika kuendeleza na kukuza taifa kwani mshindi atakayeibuka kidedea ataweza kuitangaza nchi yetu kupitia urembo wake huku akisema kuwa kauli mbiu ya mashindano hayo ni ‘Urembo na Mazingira Safi 2016’ hivyo katika kambi zao warembo wahakikishe suala la mazingira linazingatiwa kwa kufanya pia usafi.
Shindano hili limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, Golden Tulip Dar City Centre, TV1, Zan Aqua (maji ya kunywa), M&J Printing na Super Model Collections.
Na Denis Mtima/Gpl
