×

Angalia video na alichokiandika Diamond kuhusu kifo cha Papa Wemba

 

Miongoni mwa mastaa wa muziki walioguswa na kifo cha mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Papa Wemba ni Diamond Platnumz ambaye kupitia akaunti yake ya Instagram leo ametupia video inayomuonyesha akiwa na marehemu studio huko Paris nchini Ufaransa hivi karibuni.

Papa Wemba alifariki jana baada ya kuanguka akiwa stejini huko Abidjan nchini Ivory Coast alipokuwa akifanya onyesho.

Diamond kupitia Instagram ameandika hivi; “Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla nasikia habari ya msiba… Dah! nimesikitika sana, hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyezi Mungu ndiyo mpangaji…Pumzika salama, kiongozi wetu daima tutakukumbuka🙏 #RipPapaWemba”.

Kujua zaidi kuhusu Kifo na historia ya Papa Wemba ingia hapa===>>PAPA WEMBA

Leave a Comment