Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Tegeta Nyuki wakijaza kuponi zao ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Ashura Issa (kushoto) akionesha kipeperushi cha Gazeti la Uwazi baada ya kupewa na Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub.

Wadau wa Gazeti la Uwazi maarufu wa eneo la Tegeta Nyuki wakifurahia na maofisa wa Global baada ya kutua eneo hilo.

Mwanadada anayefanya biashara zake eneo la stendi ya daladala ya Tegeta Nyuki akipewa kipeperushi kutoka kwa ofisa usambazaji.

Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kulia) akimkabidhi muuza magazeti kuponi maalum ya zawadi baada ya kukutwa ameliwekea kipaumbele Gazeti la Uwazi.

Msomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Soko la Kigogo (kulia) akisaidiwa na Ofisa Masoko wa Global kukata kuponi yake.

Msomaji (kushoto) akijaza kuponi yake.

Muuzaji wa magazeti eneo la Ubungo Stendi ya Mabasi akipokea kuponi yake maalum ya zawadi baada ya kukutwa akiweka juu Gazeti la Uwazi.

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi baada ya kununua gazeti hilo na kupewa maelekezo kutoka kwa maofisa hao.

Maimuna Rashid (kushoto) akisaidiwa kujaza kuponi yake na muuzaji wa magazeti.

Muuzaji wa Gazeti la Uwazi eneo la Ubungo Stendi ya Mabasi,Halifa Rajab Nanga (kushoto) akipokea zawadi yake ya kuponi maalum kutoka kwa Ofisa Usambazaji,Jimmy Haroub.
WASOMAJI wa Gazeti la Uwazi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, jana walionekana kuvutiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendelea kutikisa hapa nchini ambayo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kupitia magazeti yake ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Wasomaji hao jana walionekana wakinunua magazeti ya Uwazi kwa wingi na kujaza kuponi ili kuwawezesha kushiriki droo ya nne ya bahati nasibu hiyo inayotarajiwa kuchezeshwa mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa upande mwingine, wauzaji wa magazeti sehemu mbalimbali za Jiji la Dar, nao walijinyakulia kuponi zenye zawadi kutoka Kampuni ya Global baada ya kukutwa wakiuza magazeti ya Uwazi.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
