×

Update: Mwili wa mtoto wa Ankal umeshawasili Dar, mazishi leo saa 10 makaburi ya Kisutu

Screen+Shot+2016-05-09+at+10.42.45+AM

Marehemu Maggid enzi za uhai wake.

Assalaam Aleikhum,

Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18),  aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini, alikukuwa masom0ni:

Mwili wa Marehemu umeshawsili  nchini jana Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa tisa  mchana kwa  ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa  ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). 

Mwili wa kijana wetu umepokelewa na wazazi, ndugu, jamaa, majirani na marafiki katika   uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.

Mazishi yamepangwa  kufanyika leo  Jumamosi saa 10  alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu  za kuandaa mazishi zitaanza  saa 4 asubuhi leo  Jumamosi, nyumbani  kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.

d67b1098-0ae4-40c6-aa5e-90bbaf982fbb Jeneza lenye mwili wa marehemu Maggid baada ya kuwasili Dar es salaam jana Ijumaa.
83945192-836d-459e-b405-b085ab6ca417Ankal akiwa na ndugu, jamaa, marafiki na badhi ya viongozi wa msikiti mara baada ya kuwasili na mwili wa marehemu katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam, ambako unahifadhiwa hadi baadae leo kabla ya kupelekwa Wazo Hill saa nne kwa dua na baadaye kurudi hapo msikitini kuswaliwa na hatimaye kupelekwa makaburi ya Kisutu kwa mazishi saa 10 Alasiri.

NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa “Twiga Cement”,  hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun

-AMIN.

Leave a Comment