Pah One
BONIPHACE NGUMIJE
Ukizungumzia wasanii wanaofanya muziki wenye swaga za ughaibuni Bongo, huwezi kuacha kuwataja wanamuziki kutoka Makundi ya Pah One na Navy Kenzo. Hii ni kwa sababu dhamira yako itakusuta hasa ukisikiliza nyimbo zao, achia mbali walizofanya pamoja kabla ya kuparaganyika kutoka mwanzo walipokuwa ndani ya kundi moja la Pah One ukiwemo Wimbo wa I Wanna Get Paid, nyimbo zao za sasa, Kamatia ya Navy Kenzo na O.T.I (Ola, Tabanako na Igwe) ya Pah One ni jibu la kila kitu.
Mbali na ukali wao, makundi haya yaliingia kwenye bifu la muda mrefu tangu walipoparaganyika. Pah One wakiwaona Navy Kenzo ‘wachawi’ kwao na Navy Kenzo wakiwaona Pah One ‘nuksi’ kwao huku kila mmoja kwa wakati wake akieleza sababu tofauti za bifu lao.
Pah One ambao mwanzoni walikuwa Ola na Ingwe kabla ya kumuongeza mdogo wao wa damu, Tabanako walisema walishindwa kwenda sawa na Aika na Nahreel (Navy Kenzo) kwa sababu washkaji hao walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi uliosababisha mambo fulani yasiende sawa. Lakini Aika na Nahreel nao walidai walishindwa kwenda sawa na jamaa hao kwa sababu ni ndugu.
Kwenye mambo mengi yakufanyia uamuzi walikuwa wakisimama upande mmoja. Bifu lao ndilo lililosababisha mpaka waanze kuwekeana vikwazo katika kutumia kazi walizofanya pamoja. Pah One wakidai kazi walizofanya zitaendelea kubaki ndani ya kundi hilo huku Nahreel akidai kazi hizo walichangia mawazo kwa hiyo zitaendelea kuwa zao wote. Jambo ‘amaizing’, sarakasi zote hizo za bifu lao sasa zimekwisha baada ya kupatanishwa hivi karibuni na kituo kimoja cha televisheni maarufu Bongo. Wao wenyewe kwa sasa wanasema, sasa kazi tu! Wasikie;
PAH ONE
Kundi hili ambalo maana ya jina lake ni ‘pamoja’ na linaloundwa na watu watatu, Ola, Igwe na Tabanako likifanya ‘interview’ na Over Ze Weekend limesema kutopatana kwao kwa muda mrefu kulitokana na Navy Kenzo kutokubali makosa yao waliyofanya mpaka wakatengana.
MSIKIE OLA:
“Kilichotutenganisha, nakumbuka wakati fulani tulikuwa na shoo Ukumbi wa Bilicanas (Posta, Dar). Sasa Aika akasema amepata matatizo anakwenda kwao, Arusha. Nahreel akadai na yeye hatakuwepo kwenye shoo kutokana na sababu zake binafsi.
“Mimi na Igwe tukatengeneza mega mix (nyimbo za kufanyia shoo) ya wawili tu. Sasa ilipofika siku ya shoo, Navy Kenzo wakaja wakidai na wenyewe wanataka kupanda stejini, sisi tulikataa kwa sababu hatukuwa tumejiandaa pamoja. Hapo ndipo walipochukia, wakaamua kujitoa.
“Lakini ninamshukuru Mungu kila kitu kimekuwa sawa, sasa tumepatana na kilichobaki ni kazi tu!”
HUYU HAPA AIKA WA NAVY KENZO:
“Ni kweli kuna makosa ya kibinadamu tulifanya, lakini nafikiri jambo la muhimu ni hili lililofanyika sasa, tumeweka mambo sawa na acha historia ijieleze.”
‘PROJECT’ YA PAMOJA
Hata hivyo, makundi haya yanatarajia kuibuka na project ya pamoja ambayo itams-hirikisha Vanessa Mdee ‘V-Money’. Pah One kwa sasa wabamba na Ngoma ya O.T.I. wakati Navy Kenzo wana Kamatia Chini.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

