×

Jide kumuanika mrithi wa Gardner Leo!

JIDEJudith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’

Stori:  Andrew Carlos, Ijumaa

Dar es Salaam: Exclusive! Lejendari wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G. Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.

HABARI ZA KUAMINIKA

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.

“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

jidenagardnerJide na Gardner

JIDE ALIPOTOKEA

Jide alifunga ndoa na Gardner Mei 14, 2005 ambapo waliishi na kufanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba, Ukumbi wa Nyumbani Lounge na Bendi ya Machozi.

FIGISUGISU NA GARDNER

Mvutano wa wawili hao ulidaiwa kuanzia kwa Jide aliyeamua kuomba talaka kwa kile kilichosemekana kuwa Gardner alipata kazi ya kutangaza redio moja nchini Kenya hivyo kama angeenda huko wakati ni meneja wake, angeshindwa kuwa naye huku pia figisufigisu nyingine nyingi zikijitokeza kama kubadilisha jina la Ukumbi wa Nyumbani Lounge na kuwa M.O.G na mambo mengine ikiwepo kusalitiana na kupigana.

WAFIKISHANA MAHAKAMANI

Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar, miezi michache iliyopita na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave a Comment