
Mshindi wa shindano la Miss Aqua Dar City Centre, Julieth Katebe akiwa katika pozi baada ya kutangazwa mshindi.

Tano Bora ya Miss Aquar Dar City Centre.

Kaimu wa nafasi ya Miss Aquar Dar City Center ambaye anamaliza muda wake, Sabina Thomas akiwa kwenye pozi. Katika mashindano yaliyopita aliibuka mshindi namba tatu.

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ akikamua jukwaani katika shindano hilo.

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Elias Barnabas ‘Barnaba Boy’ naye akifanya yake.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohanna Mkanda akiwa red carpet na mrembo.

Top Ten ya Miss Dar City Centre wakiwa kwenye pozi baada ya kutangazwa.

Wanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda na Hamisa Mobeto wakiwa kwenye pozi katika tamasha hilo.

Top 5 ya Miss Dar City Centre wakiwa kwenye pozi.

Warembo wakiwa kwenye red carpet na Miss Aquar Dar City Centre.
Stori: Boniphace Ngumije
Usiku wa kuamkia leo palikuwa hapatoshi ndani ya Ukumbi wa Mtana (Jengo la LAPF), Kijitonyama jijini Dar, kulimofanyikia shindano kubwa la warembo lililojulikana kwa jina la Zan Aqua Miss Dar City Centre.
Katika shindano hilo ambalo lilikuwa linadhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers, kulifanyika pia burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii Khalid Mohamed ‘TID’ na Elias Barnabas ‘Barnaba’ lakini pia watu waliohudhuria shindano hilo waliburudika kwa vinywaji na muziki mzuri.
“Shindano limekwenda vizuri, mshindi wetu Julieth Katebe amejinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja taslimu na nywele bandia zenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka katika kampuni ya Prima Afro, washindi wengine wamebeba zawadi mbalimbali lakini pia mshindi wa kwanza mpaka wa tano wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Miss Ilala,” alisema mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph.